Pages

Pages

Pages

Wednesday, 12 February 2014

YANGA WAIFUATA KOMOROZINE KESHO


YANGA SC inatarajiwa kuondoka kesho kwa ndege ya shirika la Precession Air kwenda Comoro kwa ajili ya mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Komorozine mwishoni mwa wiki hii.
Ofisa Habari wa klabu hiyo, Baraka Kizuguto ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba taratibu zote za safari zimekamilika, ila idadi ya wachezaji wanaondoka bado hawajaipokea kutoka benchi la ufundi.
Yanga inaondoka kesho ikiwa na matumaini makubwa ya kusonga mbele, baada ya kuichapa Komorozine mabao 7-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam Jumamosi.

Iwapo Yanga itahitimisha vyema kampeni yake hiyo, itakutana na mabingwa watetezi, Al Ahly mwezi ujao.    

<BIN ZUBEIRY>

No comments:

Post a Comment