Mbunge
wa Jimbo la Songea Mjini (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Dk Emmanuel Nchimbi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa barabara ya lami ambayo
inamaliziwa kujengwa yenye urefu wa mita 600 iliyopo katika Kata ya Mjini,
Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. Barabara hiyo imegharimu zaidi ya Sh75
milioni. Dk Nchimbi yupo mjini Songea kwa ziara ya siku tano akikagua pamoja na
kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo jimboni mwake.
Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Friday, 25 October 2013
Thursday, 24 October 2013
SIKU BOLI ZOZO ALIPOIBUKIA JANGWANI!
Kikosi cha Yanga cha mwaka 1994. Kutoka kushoto waliosimama ni Salum Kabunda 'Ninja', Constantine Kimanda, Steven Casmir Nemes, Kenneth Pius Mkapa, Selemani Mkati. Waliochuchumaa kutoka kushoto ni Nico Bambaga 'Machine', Sekilojo Chambua, Edibily Lunyamila, James Tungaraza 'Boli Zozo', na Said Mwamba 'Kizota'.
Na Daniel
Mbega
YOUNG
Africans, ambayo mwaka 1993 iliteswa sana na wapinzani wake wa jadi, Simba,
baada ya kutamba misimu miwili ya nyuma, hatimaye Jumamosi Februari 26, 1994
iliingia kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwakabili ‘wanyama hao wakali’
wa Msimbazi, ambao mwaka huo walikuwa wameongeza makucha yao kwa kuwasajili
wachezaji mahiri na wauaji wa mabingwa hao watetezi wa Tanzania Bara, Yanga.
Wednesday, 23 October 2013
MNALIKUMBUKA SCUD LA JANGWANI LILILOBOMOA MSIMBAZI MARA MBILI 1991?
Said Sued 'Scud' (wa tano kutoka kulia) akiwa na kikosi cha Yanga 1991
Na Daniel
Mbega
ZIKIWA
zimesalia siku tatu tu kabla ya pambano la Simba na Yanga, mashabiki wa timu
hizo walikuwa wamepamba moto kucharurana mitaani, lakini wadadisi wa mambo
walikuwa wamefikia uamuzi kwamba, pambano hilo lingekuwa kama fainali ya ligi
hiyo, kwa sababu, timu yoyote ambayo ingeshinda Jumamosi Agosti 31, 1991
ingekuwa vigumu kuzuiwa na timu nyingine huko mbele isitwae ubingwa wa Tanzania
Bara msimu huo.
Tuesday, 22 October 2013
MJADALA WA WAZI TAREHE 23/10/2013;MADA: UCHIMBAJI WA MADINI YA YURANI
SEMINA
ZA JINSIA NA MAENDELEO
UNAKARIBISHWA KATIKA JUKWAA LA WAZI LA MFULULIZO
WA SEMINA ZA JINSIA NA MAENDELEO (GDSS) KILA JUMATANO, AMBAPO WIKI HII MTOA MADA NI A. LUKANGA.
MADA:UCHIMBAJI WA MADINI YA YURANI KATIKA
MUKTADHA WA SOKO HURIA: JE, KATIBA MPYA ITADHIBITI UPORAJI NA KULINDA
MASILAHI YETU?
Lini: Jumatano Tarehe 23/10/2013
Muda: Saa 09:00 Alasiri – 11:00 Jioni
MAHALI: Viwanja
vya TGNP, Barabara ya Mabibo Karibu na Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji Mabibo
Sokoni
WOTE
MNAKARIBISHWA
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA
MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
[ DIWANI ATHUMANI - ACP
]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
“PRESS RELEASE” TAREHE 22. 10. 2013.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA SARE ZA
ASKARI WANYAMA PORI NA PINGU.
MNAMO TAREHE 18.10.2013 MAJIRA YA SAA
13:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA BITIMANYANGA, KATA YA MAFYEKO, TARAFA YA
KIPEMBAWE WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA
DORIA/MSAKO KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI WANYAMAPORI WALIMKAMATA SAMWEL S/O
VITALIS @ MANDE , MIAKA 34, MNYATURU, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA BITIMANYANGA
AKIWA NA SARE PAIR MOJA “KOMBATI” ZA ASKARI WA WANYAMAPORI PAMOJA
NA PINGU MOJA. MBINU NI KUTUMIA VIFAA HIVYO KATIKA UWINDAJI HARAMU.
TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUMILIKI MALI ZA SERIKALI ISIVYO HALALI
KWANI NI KOSA LA JINAI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA
JUU YA MTU/WATU AU KIKUNDI KINACHOMILIKI MALI ZA SERIKALI /WAWINDAJI
HARAMU AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAHUSIKA WAKAMATWE NA SHERIA
ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA
NA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO].
RAIS KIKWETE ATEMBELEA MGODI WA CHUMA WA LIGANGA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo
toka kwa Meneja mradi wa Maganga Matatitu Resource Development limited
Bw.
Lawrence Manyama kuhusu mlima huo uliosheheni mashapu ya chuma
alipotembelea eneo lenye utajiri wa chuma la Liganga wilaya ya Ludewa
mkoani Njombe leo
Oktoba 22, 2013.
Monday, 21 October 2013
DK. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MABUNGE YA SADC
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akiangalia vikundi vya sanaa vya ngoma za aina mbalimbali
alipowasili katika Jengo la Ukumbi wa mikutano A I C C mjini Arusha kwa
ajili ya kufungua mkutano wa siku 11 wa 34 kwa Mabunge ya Nchi wanachama
wa Jumuiya ya SADC leo Octoba 20, 2013.
YANGA FUNGA, SIMBA RUDISHA - KAMA 1996 VILE!
Picha kwa hisani ya jestina-george.com
SIMBA na Yanga zimetoka sare. Ni sare ambayo haikutegemewa
na mashabiki wa Yanga waliokuwa wanaamini timu yao ingeweza kupata ushindi wa
mabao mengi baada ya kuongoza kwa mabao 3-0 hadi timu zinakwenda mapumziko.
ZIARA YA RAIS KIKWETE WILAYANI MAKETE
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiongea
na Bi Sarah Mageni Sanga, mlemavu ambaye Rais alimpa pikipiki ya Bajaji
pamoja na mtaji wa pesa taslimu wa shilingi milioni mbili Oktoba 28,
2009 baada ya kuguswa na mkasa wa maisha ya mkaazi huyo wa kijiji cha
Lupalilo wilaya ya Makete mkoa wa Njombe alipomuona akohojiwa katika TV
na kueleza kuwa maisha yake ni magumu mno baada ya ndugu na jamaa zake
wote kuteketea kwa maradhi ikiwa ni pamoja na UKIMWI. Pichani Bi Sanga
akimshukur Rais kwa msaada huo ambao amesema umebadili kabisa maisha
yake kwani sasa anaishi kama mtu yeyote kijijini hapo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia ubora wa
shati lililotengenezwa na wanafunzio wa Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA
cha Wilaya ya Makete baada ya kukifungua rasmi chuo hicho mwishoni mwa
juma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe
kufungua rasmi Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA cha Wilaya ya Makete
mwishoni mwa juma.
Sunday, 20 October 2013
WATUMISHI WA MAHAKAMA WAASWA KUZINGATIA SHERIA, MAADILI
Naibu Waziri
wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki akisisitiza umuhimu wa kutoa adhabu
mbadala kwa watuhumiwa baada ya hukumu zao kukamilika alipokuwa anaongea na
watumishi wa Mahakama ya Mwanzo ya Kerege (hawapo pichani) iliyopo Wilayani
Bagamoyo mkoa wa Pwani kwenye ziara yake ya siku moja wilayani humo. Wa kwanza
kushoto ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa PwaniBahati Ndeserua, wa kwanza
kushoto ni Msajili Mahakama kuu, kanda ya Dar es salaam Projestus Mhagama.
Hakimu
Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo Liadi Mohamed Chamshama akimwonesha Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki (mwenye gauni kitenge) na ujumbe
wake eneo la mahakama ya Mwanzo ya Kiwangwa alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ya
siku moja wilayani mkoa wa Pwani. (Picha zote na Eleuteri
Mangi- Maelezo).
Subscribe to:
Posts (Atom)










