Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 5 October 2016

DED UBUNGO AWATAKA WATUMISHI WA MANISPAA YA UBUNGO KUZINGATIA NIDHAMU NA UADILIFU KATIKA KAZI

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Katikati) akisikiliza kwa makini maoni ya watumishi wa Manispaa hiyo wakati wa kikao cha pamoja na watumishi wa Manispaa hiyo.

WAFANYAKAZI WA GREEN WESTPRO WAICHANGIA DAMU HOSPITALI YA MUHIMBILI

Wafanyakazi wa Green WestPro wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Afisa Ustawi wa Jamii wa Hospitali ya Muhimbili, Erica Ishengoma kabla ya kuanza zoezi la kutoa damu.

Katika kusaidia na kuhakikisha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili inakuwa na akiba ya kutosha ya damu, wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green WestPro kwa pamoja wamechangia damu kwa ajili ya hospitali ya Muhimbili.

CHURA WA SNURA MUSHI ATOKA JELA, SASA MITAANI 'WATAMKOMA'!

 Snura Mushi
 Msemaji wa Msanii Snura, Baraka Nyagenda, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salamm leo.
 Msanii Snura Mushi (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeruhusu kupigwa kwa wimbo wa chura ya kuufunga kwa kuwa haukuwa na maudhui mazuri ya kitanzania. Kushoto ni Msemaji wake, Baraka Nyagenda.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

 N a Dotto Mwaibale
SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeruhusu kupigwa kwa wimbo wa chura wa msanii Snura Mushi baada ya kuufunga kwa kuwa haukuwa na maudhui mazuri ya kitanzania.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Snura Mushi alisema wimbo wake na video umeruhusiwa kupigwa baada ya audio ya chura kufanyiwa marekebisho na kuifanya kuwa katika maudhui ya kitanzania.

Alisema ruhusa hiyo imetolewa kwa barua iliyoaandikiwa Septemba 26, 2016 yenye kumbukumbu HA.26/375/01'B'/137 ambayo gazeti hili lina nakala yake.

Kupitia mkutano huo msanii Snura Mushi kwa mara nyingine aliomba radhi kwa watanzania na Serikali kwa ujumla kwa usumbufu walioupata kwa video yake ya kwanza na kuwaomba waendelee kuiona video mpya iliyorekebishwa baada ya kuifuta ya kwanza.


FAST JET YAANZISHA SAFARI ZA NDEGE MPYA NCHINI, KUANZA RASM KESHO WANANCHI WAOMBWA KUCHANGAMKIA

 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Fast Jet, John Corse (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo kuanza kutumia ndege mpya aina ya Embraer 190 kusafirisha abiria. Kulia ni Ofisa Uhusiano na Masoko wa kampuni hiyo, Lucy Mbogoro.

SIMBA YAPIGWA FAINI YA SHS. 5 MILIONI, YAAGIZWA KULIPA GHARAMA ZOTE!

Kamati ya Bodi ya Ligi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imeipiga faini ya sh. 5,000,000 (milioni tano) klabu ya Simba, kuiagiza ilipe gharama za uharibifu wa viti uliofanywa na washabiki wake katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya timu yake na Yanga iliyochezwa Oktoba Mosi mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

SERENGETI BOYS WAANDALIWA HAFLA YA KUWAPONGEZA

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge na Vijana, Dk. Abdallah Possi amesema kwamba Serikali itaendelea kusapoti michezo kwa sababu ya umuhimu wake, lakini akataka kutafutwa mbinu za kuhakikisha wadhamini wanasapoti timu za taifa na klabu mbalimbali zinazoshiriki ligi zinazosimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA MAJI ILIYOHARIBIWA NA TETEMEKO LA ARDHI.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu (kulia) akimkaribisha Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge (kulia) alipomtembelea ofisini kwake leo mjini Bukoba kujionea uharibifu wa miundombinu ya sekta ya maji iliyosathiriwa na tetemeko la ardhi.

STARTIMES YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUTAMBULISHA CHANELI MPYA

 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania,  Carter Luoh (kulia) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wa hafla fupi kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Kushoto ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Bw. Gaspa Ngowi. Katika kuadhimisha wiki hiyo StarTimes imezindua chaneli mpya tatu ambazo ni ST Bollywood Africa, ST Bollywood na FOX Life.

WATUMISHI 3 WASIMAMISHWA KAZI ARUSHA




Na Mwandishi Wetu, Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Mashaka Gambo, amewasimamisha kazi watumishi watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za uchaguzi wa mwaka 2015. 

WORLD TEACHERS’ DAY: UN SPEAKS ABOUT VALUING THEM AND IMPROVE THEIR STATUS

Message from the Heads of UNESCO, ILO, UNICEF, UNDP and Education International on the occasion of World Teachers’ Day, 50th anniversary of the 1966 UNESCO/ILO Recommendation concerning the Status of Teachers, 5 October 2016.

WAZAZI WATAKAOWAOZESHA WATOTO WAO BADALA YA KUWAPELEKA SHULE WILAYANI NZEGA KUKIONA CHA MTEMAKUNDE

 Mkuu wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula

Na Mathias Canal, Tabora
Tatizo la Mimba za utotoni na kuozesha wanafunzi katika umri mdogo limetajwa kuwa ni kikwazo kikubwa katika jamii kwani watoto wa kike wananyimwa haki ya kupata elimu ili kujikwamua na fikra mpya katika uchumi na namna ya kuwa na familia bora na endelevu katika kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

RAIS DKT MAGUFULI AMWANDALIA DHIFA YA TAIFA RAIS JOSEPH KABILA WA DRC, IKULU, DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila  Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu alikomwandalia dhifa ya Kitaifa kwaheshima yake.

TIGO YADHAMINI MBIO ZA IGOMBE CHARITY MARATHON

Mgeni rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza na wanariadha wa Tigo Igombe Charity Marathon, kabla ya kuzindua mashindano hayo yaliyofanyika mwishoni wa wiki iliyopita mjini Tabora.

DC MTATURU AWAONYA WANASIASA WANAOWAZUIA WANANCHI KUCHANGIA SHUGHULI ZA MAENDELEO


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mkunguakihendo wakati wa ziara ya kikazi.

Tuesday, 4 October 2016

DIASPORA CONFERENCE 29TH OCTOBER, 2016


You are  all  welcome  to  attend  the  above Diaspora  event  at  the  School  of  Engineering,  Coventry  University,  West Midlands,  UK
Date: 29th October 2016
Time:  From 10 .00AM
Great  Speakers on  the  Day
The Conference aspires to usher in refreshing, pragmatic discourse, implementation of initiatives and the way forward for the Diaspora in terms of harnessing our great Potential
For further information please   Tel +44 7556130219

RC SHIGELLA AFUNGUA KIKAO CHA PILI CHA BODI YA BARABARA


Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akifungua kikao cha pili cha bodi ya barabara kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.

SERIKALI YAENDELEA KUREKEBISHA MIUNDOMBINU KAGERA


Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akiongea na waandishi wa habari leo mjini Bukoba alipokuwa akitoa taarifa ya hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kurejesha hali baada ya maafa ya tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa huo.

Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba
Serikali inaendelea na juhudi za kurejesha miundombinu iliyoharibiwa na tetemeko ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za msingi za kijamii ikiwemo shule za msingi, sekondari, barabara na vituo vya afya.

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA KONGAMANO LA 30 LA KIMATAIFA LA WANASAYANSI LILILOANDALIWA NA TAASISI YA TAIFA YA UTAFITI WA MAGONJWA YA BINADAMU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR), lililoanza leo Oktoba 4 na kilelele chake kukoma Oktoba 6,2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
 .....................................................
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amelalani vikali mauaji ya watafiti WAWILI wa kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Selian cha Arusha na dereva MMOJA waliokuwa kazi katika kijiji cha Mvumi Makulu wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

KAMATI YA BUNGE LA SHERIA KUTOKA UGANDA YAFANYA ZIARA SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji (mstaafu) Salome Kaganda akiongea na Kamati ya Bunge ya Sheria  kutoka Uganda wakati wabunge hao walipofanya ziara ya kujifunza jinsi Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma inavyofanya kazi hasa Baraza la Maadili linavyofanya kazi. (Picha na Benjamin Sawe-Maelezo)

MALINZI: SITAWAACHA SERENGETI BOYS

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema kwamba ataendelea kuwa karibu na vijana na Timu ya Tanzania ya vijana ‘Serengeti Boys’ licha ya kuondolewa na Congo kwenye harakati za kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana zitakazofanyika Madagascar, hapo Aprili, mwakani.

ETHIOPIA YAFUTA MCHEZO DHIDI YA TAIFA STARS

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea barua kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Ethiopia (EFF), ikielezea juu ya kufutwa kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliokuwa ufanyike Oktoba 8, 2016.

MAKAMU WA RAIS WA CUBA AMALIZA ZIARA YA SIKU TATU YA KIKAZI NCHINI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akiagana na mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Antonio Valdes Mesa ambaye amemaliza ziara ya siku 3 ya kikazi nchini.
                                          ............................................................
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa ameondoka nchini mchana huu baada ya kumaliza ziara ya kiazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. 

BANDA LA MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA) LAVUTIA WENGI KATIKA MAONESHO YA WAJASIRIMALI KANDA NYANDA ZA JUU KUSINI


Kaimu Meneja huduma kwa wateja na Elimu kwa Umma Ndugu Jemsi Ndege akitoa elimu kwa wajasilimali na wananchi waliofika katika banda la Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)Katika maonesho ya wajasilimali Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yaliyoandaliwa na SIDO katika viwanja vya bustani ya jiji la Mbeya.

SBL KUWAPATIA MAJI BURE WAKAZI 65,000 WA TEMEKE, ARUSHA

Moja ya Mradi wa maji uliodhaminiwa na SBL Wilaya ya Hanang mkoani Manyara
Dar es Salaam, Oktoba 04, 2016 – Takribani wakazi 65,000 wa maeneo ya Temeke mkoani Dar es Salaam na Likamba mkoani Arusha  hivi karibuni wataanza kufurahia  upatikanaji wa  maji safi na salama bure  huduma  ambayop itatolewa na kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).

CHAMA CHA WATU WENYE UALIBINO MKOANI MWANZA CHATOA KILIO CHAKE KWA RAIS MAGUFULI

Na BMG
Chama cha watu wenye ualibino mkoani Mwanza, kimemuomba Rais John Pombe Magufuli, kukemea vikali vitendo vya ukatili ikiwemo kutekwa na kuuawa kwa watu hao kama anavyokemea masuala ya rushwa na ufisadi kwenye mikutano yake mbalimbali.

"MRADI WA GREEN VOICES UMEONYESHA MAFANIKIO, UTAWAKOMBOA WANAWAKE TANZANIA"



Makamu wa Rais mstaafu wa Hispania na Rais wa Taasisi ya Women for Africa Foundation, Mama Maria Tereza Fernandez de la Vega, akisalimiana na maofisa wa ulinzi na usalama mara baada ya kuwasili katika bandari ya Nansio, Ukerewe hivi karibuni kuzindua mradi wa kilimo cha viazi lishe unaofadhiliwa na taasisi yake ya inayoshughulikia maendeleo ya Wanawake wa Afrika.
Mama Getrude Mongella (waliosimama katikati mwenye blauzi nyekundu) akifafanua jambo kwa Mkamu wa Rais mstaafu wa Hispania na Rais wa Taasisi ya Women for Africa Foundation, Mama Maria Tereza Fernandez de la Vega, wakati walipotembelea mradi wa kilimo cha viazi lishe wilayani Ukerewe. Kushoto kwa Mama Mongella ni Bi. Leocadia Vedastus, ambaye ni mshiriki kiongozi wa mradi huo.
Makamu wa Rais mstaafu wa Hispania na Rais wa Taasisi ya Women for Africa Foundation, Mama Maria Tereza Fernandez de la Vega, akiangalia bidhaa zilizo mbele yake ambazo zinatokana na viazi lishe katika kuongeza mnyororo wa thamani. Hii ni wakati alipokwenda kuuzindua mradi huo wilayani Ukerewe katika Mkoa wa Mwanza.
MRATIBU wa mradi wa akinamama wapambanao na mazingira wa Green Voices, Alicia Cebada, amesema kwamba wamefarijika na mradi huo kwa kuwa umeonyesha mafanikio makubwa nchini Tanzania.

Monday, 3 October 2016

WAFADHILI WAFURAHISHWA NA UKAUSHAJI WA MBOGA MBOGA




Mkurugenzi wa mawasiliano wa taasisi ya Mfuko wa Wanawake Afrika, Anna Salado (kulia), akipakua mboga zilizopikwa kiasili na kuungwa kwa nazi wakati yeye na ujumbe wake walipotembelea mradi wa ukaushaji wa mboga na matunda wa wanawake wa Kata ya Mzinga mkoani Morogoro hivi karibuni. Kushoto ni Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro, Milikieli Mansweat Mahiku.

Mratibu wa mradi wa Green Voices kutoka taasisi ya Mfuko wa Wanawake Afrika ya Hispania, Alicia Cebada, akiwa ameshikilia pakiti ya kisamvu kilichokaushwa na kufungashwa huku akiwapongeza wanawake wa kikundi cha Mzinga katika Kata ya Mzinga, Manispaa ya Morogoro kwamba wamefanya kazi nzuri sana. Mwenye fulana nyeupe ni Bi. Esther Muffui, mshiriki kiongozi wa mradi huo.

SIYO tu mapishi ya asili ya kisamvu kikavu kilichoungwa kwa nazi, lakini mafanikio makubwa katika ukaushaji na usindikaji wa mboga na matunda katika mradi wa wanawake wa Kata ya Mzinga, Manispaa ya Morogoro yamewavutia wahisani wa taasisi ya Women for Africa Foundation kutoka Hispania.
Hali hiyo imewafanya wanawake hao wawe katika nafasi kubwa zaidi ya kusonga mbele ikiwa wafadhili hao watatoa tena fedha katika awamu ya pili ya mradi wa Green Voices unaotekelezwa nchini Tanzania.

Sunday, 2 October 2016

ACT YAZINDUA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA JIJINI DAR

Mchungaji wa Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele akisali wakati akifungua Ibada hiyo iliyokuwa ni ya ufunguzi wa Harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa Kanisa.

Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) linaloendesha shughuli zake katika ukumbi wa Utoji, Sinza Mapambano jijini Dar limezindua harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo rasmi .

MKUU WA MKOA WA MWANZA ATAKA MAHAKAMA KUREJESHA IMANI KWA WANANCHI



Na George Binagi-GB Pazzo @BMG
Watendaji wa Mahakama nchini wamehimizwa kufanya kazi kwa uwazi na uadilifu, ili kurejesha imani kwa wananchi juu ya chombo hicho muhimu katika utoaji wa maamuzi.

TAASISI ZAENDELEA KUTOA MISAADA KAGERA

Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawiro akiwashukuru Taasisi ya Kimataifa ya Lions Club ya jijini Mwanza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu na kusema kuwa mahitaji kwa waathirika wa tetemeko la ardhi bado ni makubwa na misaada inahitajika ili kuwasaida waathirika hao.

WANAFUNZI WA IHUNGO NA NYAKATO WAANZA KUWASILI WALIPOPANGIWA

 Mkuu wa Wilaya ya Bukoba (DC) Deodatus Kinawiro (wa kwanza kushoto) akitembelea maeneo mbalimbali katika Chuo cha Ualimu cha Bukoba kinachomikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (BLTC) kinachomolikiwa na Dayosisi ya Kaskazini Magharibi ambapo wanafunzi wa kidato cha tano kutoka shule ya sekondari Ihungo wataenda kusoma wakati shule yao inajengwa upya baada ya kuharibiwa kwa tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10, mwaka huu. Wa kwanza kulia ni Mkufunzi katika chuo hicho Dafroza Protas.

BODI YA TAIFA YA WAHASIBU NA WAKAGUZI WA HESABU (NBAA) YAFANYA MAHAFALI YA 38

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Kulia, akiwahutubia wahitimu na jumuiya ya Bodi ya taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) (Hawako Pichani), wakati wa mahafali ya 38 ya Bodi hiyo, yaliyofanyika katika Kituo cha Bunju, Nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam, kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, Bw. Pius Maneno na Mwenyekiti wa kamati ya Elimu na Mafunzo wa Bodi hiyo, Bi. Anne Mbughuni.

LHRC YATOA TAMKO KWA VYOMBO VYA HABARI SIKU YA WAZEE DUNIANI

Dkt.Helen Kijo-Bisimba
OKTOBA Mosi (1) ya kila mwaka ni siku iliyoteuliwa na Umoja wa Mataifa kuadhimisha uwepo wa wazee katika jamii kote ulimwenguni. Siku hii ilianza kuadhimishwa rasmi Oktoba 1, 1991 kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu mambo yanayowalenga wazee ikiwemo kutoheshimu haki za wazee, kutazama mahitaji na maslahi ya wazee na kuhakikisha mzee popote alipo ulimwenguni anapata huduma za msingi za kijamii kama vile huduma bora za afya na matibabu. 

AMIRI JESHI MKUU RAIS DKT. MAGUFULI ALIPOFUNGA MAFUNZO YA MEDANI YA KIJESHI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akilakiwa na Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Jenerali Davies Mwamunyange alipowasili kushuhudia kufungwa kwa  mafunzo ya medani ya Kijeshi ya kutua ardhini kutoka majini  (Amphibous Landing) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ, katika kijiji cha Baatini, Wilayani Bagamoyo.

ASKARI POLISI APATWA KIGUGUMIZI KUSIMAMIA SHERIA

 Askari Polisi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), akipiga picha gari lenye namba T 297 AQE baada ya dereva wa gari hilo kukiuka sheria ya usalama barabarani kwa kusimama kwenye reli katika makutano ya reli na barabara ya Nyerere eneo la Gold Star jijini Dar es Salaam majira ya saa sita mchana leo gari hilo lilikuwa likitokea maeneo ya Mnazi Mmoja lilielekea Tazara. 

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza katika eneo la JKT Mgulani ambapo shughuli za uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika jiji la Dar es Salaam zilifanyika.

RC MONGELLA AFUNGUA MKUTANO WA ROBO MWAKA WA CHAMA CHA MAJAJI NA MAHAKIMU MIKOA MWANZA NA GEITA

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella, akizungumza kwenye Ufunguzi wa Mkutano wa Robo Mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu JMAT, tawi la Mwanza na Geita, unaofanyika leo kwenye ukumbi wa jengo la NSSF Jijini Mwanza.

MASAUNI AZITAKA TAASISI ZA KIDINI NCHINI KUPAMBANA NA MAOVU, AFUNGUA MKUTANO WA 47 WA JUMUIYA YA WAISLAMU WA AHMADIYYA

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), Rais Mstaafu awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi wakiwapungia waumini wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya (hawapo pichani) wakati walipokuwa wanawasili katika Ukumbi wa Mkutano wa Jumuiya hiyo, uliopo Kitongoji cha Kitonga, Kata ya Msongola, Ilala, jijini Dar es Salaam. Masaunia ambaye alikuwa mgeni maalum katika mkutano huo wa 47 wa jumuiya hiyo nchini, aliitaka Jumuiya hiyo pamoja na Taasisi zingine za kidini nchini kuendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii kwa kuwapatia waumini wao elimu na maarifa ya kuboresha tabia na maadili yao kiroho. Kulia ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya hiyo nchini, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.