Pages

Pages

Pages

Friday 9 December 2016

MASAUNI AWAPA HAMASA WACHEZAJI TIMU YA MIEMBENI, YAPAMBANA NA TAIFA JANG’OMBE LIGI KUU ZANZIBAR, ZATOKA SARE UWANJA WA AMANI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wachezaji wa Timu ya Mpira wa Miguu, Miembeni Club kabla ya timu hiyo kupambana na Timu ya Taifa Jang’ombe katika Uwanja wa Amani, Zanzibar. Masauni aliwaambia wachezaji wa Timu hiyo inayotoka katika Jimbo lake, wajitume na wahakikishe ushinde unapatikana. Hata hivyo timu hizo zilitoka sare kwa kufungana goli moja kwa moja. Picha na MOHA.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto aliyevaa kofia) akiwa na Katibu wa Timu ya Miembeni, Simai Mwalimu wakiingia ndani ya Uwanja wa Amani, Zanzibar kwa ajili ya kushuhudia timu hiyo inayotoka katika Jimbo la Masauni, ikipambana na Timu ya Taifa Jang’ombe katika  mzunguko wa Ligi Kuu visiwani humo. Picha na MOHA.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiwa na Katibu wa Timu ya Miembeni, Simai Mwalimu wakiangalia wachezaji wa Timu ya Miembeni (hawapo pichani) ilipokuwa inafanya mashambulizi dhidi ya Timu ya Taifa Jang’ombe katika mzunguko wa Ligi Kuu ya Zanzibar zinazofanyika katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja. Timu hizo zilitoka sare kwa kufungana goli moja kwa moja.  Picha na MOHA.

No comments:

Post a Comment