Pages

Pages

Pages

Thursday 15 September 2016

MASHINDANO YA MGIMWA CUP YAZINDULIWA RASMI NA DC WA MUFINDI JUMHURI WILLIAM

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jumhuri William, akipiga mpira katika eneo la penati kuashiria kuwa mashindano ya Mgimwa Cup yamezinduliwa rasmi.

 Mkuu wa Wilaya Mufindi, Jumhuri William, aliyeshika mpira kulia sambamba na Mwenyekiti wa CCM Mufindi Yohanes Kaguo aliyeshika mpira kushoto wakiwa na baadhi ya wachezaji.
 Mkuu wa Wilaya Mufindi, Jumhuri William, akikagua timu kabla mtanange kuanza.

  Mkuu wa Wilaya Mufindi, Jumhuri William, akikagua timu kabla mtanange kuanza huku akiwapa neno wachezaji wa timu husika katika kiwanja cha Ikwea.


Na Fredy Mgunda, Iringa 

MASHINDANO ya Kombe Mgimwa yamezinduliwa rasmi katika Kijiji cha Ikwea Kata ya Ikwea wilayani Mufindi mkoani Iringa kwa kushirikisha timu za vijiji vyote vya jimbo la mfundi kaskazini kwa lengo la kuinua vipaji wa wachezaji wa jimbo hilo.

Akizindua mashindano hayo yaliyofanyika Kiwanja cha Ikwea katika kijiji cha Ikwea mkuu wa wilaya Jumhuri William kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini alisema ni wakati mzuri kwa sasa kuyageukia mashindano ya mchangani kwani yamesheheni vipaji vingi vitakavyosaidia kuendeleza mpira wa Tanzania wakati ambapo taifa likiendelea kupata matokeo yasiyoridhishwa kwenye soka kwa sasa.

"Mashindano haya ni muhimu sana kwa wakati huu kwani yatasaidia kuinua vipaji vya vijana wetu na kuweza kupata timu bora ya taifa hivyo nidhamu ni muhimu wakati wa michezo hiyo," alisema William.

Aidha, William aliongeza kwa kusema kuwa mpira wa miguu umekuwa na faida kwa wachezaji kwani wanaweza kujitengezea vyanzo vya ajira kama Mbwana Samatta na wachezaji wengine walipwa vizuri saizi hapa nchini hata nje ya nchi.

 “Soka imewapa ajira mamilioni ya wachezaji na viongozi ulimwenguni na wameweza kuishi maisha ya kifahari kutokana na mishahara wanayopata,” alisema William.
   
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo Felix Nyimbo aliwataka washiriki wa mashindano hayo kujituma ili ipatikane timu ya kata ambayo itakuwa ikiwakilisha kata hiyo katika mashindano ya wilaya, kanda hadi taifa.

“Mwaka huu tumekuja na wataalamu wanachagua vipaji maalumu kwaajili ya kujiunga na timu yetu ya kurugenzi ya mafinga na lengo likiwa ni kuhakikisha vipaji vyote vya Jimbo la Mufindi Kaskazini vinaonekana na vinafika mbali kwa kuwa sasa mpira ni ajira si mnamuana mchezaji Mbwana Samatta,” alisema Nyimbo.

Kwa upande wake mlezi wa mashindano hayo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Mufindi Yohanes Kaguo alisema ataendelea kwaunganisha vijana kupitia michezo na kusaidia kukuza mpira wa Wilaya ya Mufindi.

“Ilani ya Chama cha Mapinduzi inatutaka wenyeviti kote nchini kuhakikisha michezo inafanyika mara kwa mara na kuleta tija kwa taifa ili tuondokane kuwa kuwa vichwa vya wendawazimu,”alisema Kaguo.

Mashindano ya Mgimwa Cup ni miongoni mwa mashindano yanayolenga kuibua vipaji vya vijana vijijini ili kuwawezesha kupata nafasi ya kucheza katika vilabu vikubwa nchini.

No comments:

Post a Comment