Pages

Pages

Pages

Monday 9 May 2016

TANZIA: ANKAL MICHUZI AFIWA NA MWANAYE

Ankal Issa Michuzi anasikitika kutangaza kifo cha mwanaye Maggid Muhidin kilichotokea jana Jumapili huko Durban, Afrika Kusini, alikokuwa masomoni.

Mipango ya kuusafirisha mwili wa marehemu inafanywa, msiba utakuwa Tabata Mawenzi jijini Dar es Salaam ambako ratiba ya mazishi itatoka mara tu baada ya mwili kuwasili.

Habari ziwafikie ndugu, jamaa, majirani na marafiki popote pale walipo.

Innalillah wa inna ilayhi raajiun

No comments:

Post a Comment