Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 14 May 2016

SERIKALI YATOA BILIONI 2.3 KUWALIPA WAFANYAKAZI WA NIDA


Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
13/05/2016. Dar es salaam.

Serikali imeipatia Mamkala ya Vitambulisho vya Taifa NIDA shilingi bilioni 2.3 (Bilioni mbili na milioni mia tatu) kwa ajili ya kuwalipa watumishi wa muda 597 wa mamlaka hiyo waliosimamishwa kazi hivi karibuni.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango leo jijini Dar es salaam imesema kuwa malipo hayo yanahusisha mishahara yao ya miezi minne na mshahara wa mwezi mmoja wa notisi ya kusimamishwa kazi pamoja na malimbikizo ya madeni yao katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa kabla ya kuwalipa watumishi hao  Wizara ya Fedha ilifanya uhakiki wa mahojiano ya ana kwa ana na watumishi hao pamoja na kupitia nyaraka mbalimbali zikiwemo majalada, mikataba ya ajira na madaftari ya mahudhurio, taarifa za kazi za kila siku pamoja na namba zao za akaunti ya benki zilizokuwa zikitumika kulipia mishaara ili kujidhihirisha kama madai hayo yalikuwa sahihi.

Mbali na hayo taarifa hiyo imeeleza kuwa katika uhakiki huo wizara ilibaini kulikuwa na kasoro kadhaa za kimikataba kati ya NIDA na watumishi hao.

Aidha,imeeleza kuwa wakati wa zoezi hilo jumla ya watumishi 597 walipaswa kuhakikiwa na kuongeza kuwa majina 565 ndio yaliyowasilishwa kuhakikiwa ambapo watumishi 516 walijitokeza katika zoezi hilo na watumishi 49 hawakujitokeza.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Watumishi 472 kutoka Tanzania bara na Tanzania visiwani ndio waliokidhi vigezo vya kulipwa stahili zao za kuachishwa kazi huku 121 wakibainika kuwa na kasoro mbalimbali ambazo zinapaswa kurekebishwa na Menejimenti ya NIDA kabla ya malipo hayo.

Ikizitaja baadhi ya kasoro hizo zilizobainika katika ukahiki huo ni pamoja na kusekana kwa mikataba na majalada yao katika Ofisi ya mwajiri, kukosekana kwa majina yao kwenye daftari la mahudhurio kazini, kuwa na utata kwenye mikataba, kufanana kwa namba za majalada na kukosekana kwa barua za kusitishwa kazi.

Kufuatia uhakiki huo, Wizara ya Fedha na Mipango imemaliza kazi yake ya Uhakiki na kwamba jukumu la kuwalipa watumishi wa NIDA wanaostahili limeachwa mikononi mwa Menejimenti ya NIDA.

No comments:

Post a Comment