Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 14 May 2016

SERIKALI KUWAWEZESHA WANAWAKE KATIKA SEKTA YA MADINI


FRANK MVUNGI- Maelezo

Serikali imejipanga kuimarisha kituo cha Jimolojia kilichopo Jijini Arusha ili kufundisha na kuzalisha vijana wa kitanzania ili waweze kusanifu na kung’arisha madini ya vito.Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar  es salaam na Kaimu Kamishna wa Madini  Mhandisi Ally Samaje wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kutoa tathmini ya maonesho ya tano ya kimataifa ya madini ya vito yaliyofanyika jijini Arusha mwezi Aprili 2016.

“Tayari vijana wa kike 29 wameshapatiwa mafunzo ya miezi 6 ya ukataji wa madini ya Vito kwenye kituo chetu cha Jimolojia na Wengine 18 wanaendelea na mafunzo ya miezi 6 yaliyoanza mwezi machi 2016” alisisitiza Samaje

Akifafanua zaidi Mhandisi Samaje amesema Serikali ya awamu ya tano inayo dhamira ya dhati katika kuwainua vijana wa kike kwa kuwajengea uwezo wa kushiriki katika ukataji wa madini na kuyaongezea thamani ili wachangie katika kukuza uchumi wa Taifa kupitia sekta ya madini.

Aidha Samaje amebainisha kuwa Serikali inaompango wa kuanzisha ukanda maalum wa uwekezaji (EPZ) katika eneo la Mererani ambapo shughuli za biashara ya madini na uongezaji thamani ya madini ya Tanzanite zitakafanyika kwa uhuru na uwazi.

Pamoja na juhudi hizo Serikali itaendelea kudhibiti vitendo vya utoroshaji wa Madini nje ya nchi yakiwemo Tanzanite kwenye viwanja vya ndege na kwenye migodi ambapo madini yanazalishwa.

Pia Samaje alitoa wito kwa wachimbaji na wananyabiashara wa madini nchini kuzingatia Sheria zilizopo wakati wa kufanya shughuli zao ili  waweze kuchangia katika kukuza uchumi wa Taifa.

Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara wa madini Tanzania (TAMIDA) iliendesha maonyesho ya tano ya kimataifa ya Madini ya vito yaliyofanyika jijini Arusha Mwezi April,2016.maonyesho haya hufanyika kila mwaka Jijini Arusha na kukutanisha washiriki mbalimbali wakiwemo wachimbaji,wafanyabiashara wa madini wa ndani na nje,na wataalam mbalimbali wenye uzoefu wa shughuli za madini ya vito.

No comments:

Post a Comment