Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 9 May 2016

KUZIONA MBEYA CITY VS YANGA NI BUKU TANO TU!

Maandalizi ya mchezo namba  218  wa ligi kuu ya soka Tanzania  bara  kati ya Mbeya City fc na Yanga ya Dar es Salaam uliopagwa  kuchezwa kesho kwenye uwanja wa Sokoine  jijini hapa yamekamilika  kinachosubiriwa ni dakika 90 hapo kesho.

Kwa mujibu wa msimamizi wa kituo cha Mbeya ambaye pia ni katibu mkuu wa chama cha soka mkoa, Haroub Suleiman, mchezo huo  utafanyika kama ulivyopangwa kwa sababu timu zote mbili tayari zisharipoti (kuwepo) kituoni na tayari makubaliano juu ya kiingilia  yashafikiwa.
“Yanga wamewasili asubuhi ya leo, hii ina maana kuwa mchezo  upo kama ulivyopangwa, kutokana na uzito wa mchezo wenyewe,tumekubaliana kiingilio kitakuwa  shilingi 5000, nawaomba mashabiki wote wa soka katika kanda  hii ya nyanda za juu kusini  wajitokeze kwa wingi  kuzishangilia timu zao huku pia  wakitakiwa kudumisha amani kabla na baada ya mchezo” alisema.
Kwa upande wake  Mwenyekiti wa Mbeya  City Fc, Mussa Mapunda amewatakia kila la kheri na kuwashukuru mashabiki wote wa timu yake popote walipo ndani na nje ya nchi kwa jinsi walivyojitolea  kuisapoti  timu yao tangu ilipopanda daraja  na kuwataka  kujitokeza kwa wingi hapo kesho  kuja  kuisapoti na kushuhudia  City ikiandikisha  ushindi wa kwanza mbeya ya Yanga.
“Pambano hili nalifananisha  na lile la ki’ Biblia linalowahusu Daud na Goliatti, kwa kila hali tumepania  ili tuibuke na ushindi, lakini ushindi wetu utaletwa pia na mshikamano kutoka pande zote tatu kwa maana ya uongozi, wachezaji na mashabiki, tumeiandaa timu vizuri na najua  mashabiki wetu wako tayari muda wote,naomba wajitokeze kwa wingi  waje na mashamsham ya kila namna  ili kuhakikisha tunashinda mchezo huo, Nyumbani kwanza, Objective to win” alisema.

No comments:

Post a Comment