Pages

Pages

Pages

Thursday 26 May 2016

CAF YAMTEUA MICHAEL WAMBURA KUWA KAMISHNA

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), limemteua Michael Richard Wambura (pichani) kuwa Kamishna wa mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Rwanda na Msumbiji unaotarajiwa kufanyika jijini Kigali, Juni 3, 2016.
Wambura ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), atakuwa Balozi mzuri katika mchezo huo unaokutanisha timu ambazo nchi imepana nazo. Msumbiji iko Kusini mwa Tanzania wakati Rwanda iko Magharibi mwa Tanzania.

No comments:

Post a Comment