Pages

Pages

Pages

Friday 1 April 2016

WATUMISHI HEWA 2,204 WALAMBA ZAIDI YA SHS. 5 BILIONI KWA MWAKA

Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene (kushoto) akipokea taarifa ya watumishi hewa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Felix Ntibenda (kulia) hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo na katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Mussa Iyombe.

TAKRIBAN watumishi 2,204 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara wamekuwa wakiitia hasara serikali ya Shs. 5.5 bilioni kila mwaka, brotherdanny.com inaripoti.

Hayo yamebainishwa katika majumuisho ya awali ya ripoti za wakuu wa mikoa zilizowasilishwa kwa Waziri wa Nchi (Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), George Simbachawene, jijini Dar es Salaam Aprili Mosi, 2016 wakiitikia agizo la Rais John Magufuli la kufanya uhakiki wa watumishi hewa.
Hata hivyo, ni Mkoa wa Shinyanga pekee ambao ubeinika kutokuwa na watumishi hewa kutokana na mikakati iliyowekwa tangu Julai 2014 na mkuu wa mkoa aliyepita.
Inaonyesha kwamba, Mkoa wa Arusha ndio unaoongoza kwa sasa kwa kuwa na watumishi hewa 270 ambao katika kipindi cha mwaka mmoja wamelamba kiasi cha Shs. 1.8 bilioni ambazo ni fedha za walipa kodi.
Mkuu wa mkoa huo, Daudi Felix Ntibenda, amesema katika zoezi hilo wamebaini idadi hiyo ya watumishi hewa, ambao wamekuwa wakiitia hasara serikali kila mwaka.
“Mheshimiwa, katika zoezi letu tumebaini kwamba wapo watumishi hewa 270 ambao wamekuwa wakiisababishia serikali hasara ya Shs. 1.8 bilioni kila mwaka,” alisema.
Kwa upande mwingine, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alisema zoezi la awali la uhakiki limebaini kuwepo kwa watumishi hewa 73 ambao wamesababisha serikali ipoteze kiasi cha Shs. 316 milioni kila mwaka.
“Katika mkoa huu tumepata watumishi hewa 73, lakini wengi watahoji kwa nini mkoa huu mkubwa wenye idadi kuzwa ya watu na taasisi za umma una idadi ndogo ya watumishi hewa, nataka nikuhakikishie tu Mheshimiwa Waziri, bado tunaendelea na uchunguzi wetu wa kina,” alisema Makonda.
Katika Mkoa wa Dodoma, wamegundulia watumishi hewa 101 na kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa huo, Jordan Rugimbana, watumishi hao hewa wameisababishia serikali hasara ya Shs. 287.3 milioni katika kipindi cha miezi sita tu iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, amesema katika mkoa wake wamegundua kuwepo kwa watumishi hewa 15, lakini akasema kuna watumishi wengine 145 ambao hajaonana nao.
“Mheshimiwa Waziri, idadi hii inaweza kuongezeka kwa sababu wao watumishi wengine 145 ambao sijaonana nao, bado tunaendelea na zoezi kuwabaini pamoja na kujua kiasi cha hasara ambacho wameisababishia serikali,” alisema.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (mstaafu) Salum Kijuu amesema mkoa wake wamebaini kuwepo kwa watumishi hewa  14 ambao wamesababisha upotevu wa fedha za serikali Shs. 49.1 milioni.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Jenerali Raphael Muhuga, kwa upande wake amesema wamegundua kuwepo kwa watumishi hewa 21 ambao wameitia serikali hasara ya Shs. 20.7 milioni.
Naye Mkoa wa Kigoma, Bregedia Jenarali (mstaafu) Emmanuel Maganga amesema mkoa huo umebaini kuwepo watumishi hewa 171 ambao wameitia serikali katika hasara ya Shs. 114.6 milioni.
Said Meck Sadick, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, amemweleza Waziri Simbachawene kwamba, ndani ya mkoa huo wamebaini kuwepo kwa watumishi hewa 111 ambao wameisababishia hasara ya Shs. 281.4 kwa serikali.
Mkuu waa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, amesema mkoa wake una watumishi hewa 57 ambao wameitia hasara serikali Shs. 36.2 milioni.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera, amesema mkoa huo umegundua kuwepo kwa watumishi hewa 42 ambao wameitia hasara serikali Shs. 313.9 milioni.
Katika Mkoa wa  Mara, mkuu wa mkoa huo, Magesa Mulongo, amesema wamebaini kuna watumishi hewa 94 mkoani humo ambao wameitia hasara serikali Shs. 121 milioni.
Kwa upande wa Mkoa wa Mbeya, Mkuu wa Mkuo huo, Amos Makalla amesema wamegundua kuwepo kwa watumishi hewa 98 ambao wameitia hasara serikali Shs. 459 .6 milioni kwa mwaka.
Kwenye Mkoa wa Morogoro, mkuu wa mkoa huo, Dk. Steven Kebwe, amesema mkoa wake umegundua kuwepo kwa watumishi hewa 122 ambao wameitia hasara serikali Shs. 450.7 milioni.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu, amesema mkoa wake ubaini kuwepo kwa watumishi hewa 17, huku watumishi wengine 285 uchunguzi ukiendelea.
“Watumishi hao 17 wameitia hasara serikali Shs. 216.5 milioni,” alisema Dendegu.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema mkoa wake umengundulika kuwa na watumishi hewa 334.
Mkuu wa Mkoa wa NJombe, Dk. Rehema Nchimbi, amesema mkoa wake umegundulika kuwa na watumiwa na hewa 34 ambao amesema wamekuwa wakiitia hasara serikali Shs. 20.1 milioni kila mwaka.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, amesema mkoa wake umekuwa na watumishi hewa 150 huku hakishindwa kusema hasara ya fedha za serikali kwa madai kuwa uchunguzi unaendelea.
Katika Mkoa wa Rukwa, mkuu wa mkoa huo Kamishna Mstaafu Zerote Steven, amesema mkoa wake umekuwa na watumishi hewa 18 na wametia hasara serikali Shs. 55.6 milioni.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Thabit Mwambungu, amesema mkoa huo umebainika kuwa na watumishi hewa 35 ambao wameitia hasara serikali Shs. 58.4 milioni.
Mkuu wa Mkoa Simiyu, Antony Mtaka, amesema mkoa huo umegundulika kuwa na watumishi hewa 62 ambao wameitia hasara serikali ya Shs. 320.9 milioni.
Katika Mkoa wa Singida, mkuu wa mkoa huo, Mhandisi Mathew Mtigumwe, amesema wafanyakazi hewa waliobainika mkoani kwake ni 231 na kueleza kuwa uchunguzi bado unaendelea ili kubawaini zaidi na kujua kiasi cha hasara waliyoisababishia serikali.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, amesema katika mkoa wake watumishi hewa waliobainika ni 48 ambapo wanaitia hasara serikali Shs. 118.7 milioni.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela, amesema watumishi hewa waliobainika mkoani humo ni 104 ambapo amesema tathmini ya kuhakiki bado inaendelea.

No comments:

Post a Comment