Pages

Pages

Pages

Friday 11 March 2016

UJUMBE MZITO WA ACT WAZALENDO KUMKARIBISHA RAIS WA VIETNAM


TAARIFA KWA UMMA
KARIBU TANZANIA RAIS TRUONG SANG WA VIETNAM

Chama cha ACT Wazalendo kinaipa uzito wa kipekee ziara yakwanza nchini na barani Afrika ya rais wa taifa la Kisoshalisti la Vietnam Truong Sang anayezuru Tanzania kuanzia siku yaJumatano tarehe 9 Machi, 2016.
Kwetu Chama cha Wazalendo, Vietnam ni mfano wa kuigwa nanchi zinazoendelea juu ya umuhimu wa sera bora na usimamizithabiti wa rasilimali katika kuipaisha nchi kiuchumi.
Tanzania na Vietnam zilipopata uhuru, zilikuwa katika kiwangokinachokaribiana kiuchumi. Sasa Vietnam imesonga mbelekiuchumi mara dufu zaidi ya Tanzania karibu kwenye kilanyanja.
Mifano ni mingi: Vietnam iliyokuja kuchukua mbegu nakujifunza upandaji wa mikorosho nchini Tanzania ndiyo nchiinayoongoza duniani kwa uzalishaji wa korosho ghafi kwa sasa. Tofauti na Tanzania ambayo huuza sehemu kubwa ya koroshozake zikiwa ghafi, nchini Vietnam korosho hubanguliwa kablaya kuuzwa ndani na nje ya nchi ili kuziongezea thamani.
Haya yamewezekana kwa sababu, pamoja na mambo mengine, Vietnam imewekeza katika uendelezaji wa teknolojia rahisi yaubanguaji wa korosho vijijini ambapo korosho zinabanguliwavijijini zinakozalishwa na kuongeza ajira.
Pia, Vietnam iliyokuja kuchukua mbegu ya kahawa Tanzania ndiyo nchi ya pili kwa uzalishaji wa kahawa duniani kwa sasaikitanguliwa na Brazil. Vietnam imewahi pia kuchukua samakiaina ya Sato ili kuendeleza sekta yao ya uvuvi. Swali la kujiuliza, sisi tunachukua nini kutoka Vietnam?
Vietnam inafanya vyema zaidi pia kwenye maeneo ya viwanda, usalama wa chakula, teknolojia ya mawasiliano na ustawi wawatu wake.
Wakati Tanzania ikikumbatia masharti ya soko huria nakubinafsisha kiholela viwanda, mashamba ya umma namakampuni kwa maelekezo ya mashirika ya fedha ya kimataifa, Vietnam ilibuni mfumo wake wa mageuzi ya kiuchumi (“DoiMoi”) unaovutia mitaji binafsi ili ishindane na mitaji ya dola.
Maono na msimamo wa kiuchumi wa ACT Wazalendo daimaumekuwa ni ujenzi wa uchumi unaostawisha sekta binafsi bilakuathiri jukumu la dola kuhodhi sekta nyeti za kiuchumi kwamanufaa ya umma.
Ziara ya Rais wa Taifa la kijamaa la Vietnam ifumbue macho serikali ya CCM kutoka kwenye maneno matupu ya uchumi waviwanda na kwenda kwenye vitendo. Mawaziri wa CCM wamekuwa wakiendelea kutoa ahadi za ujenzi wa viwanda kana kwamba bado tupo kwenye kampeni.
Chama cha ACT kinawashawishi wananchi kuhitaji utekelezaji wa ahadi sasa.
Tunachukua fursa hii kukukaribisha sana Tanzania Rais Truong Sang.
Imetolewa leo tarehe 9, Machi 2016.
Ado Shaibu,
Katibu, Itikadi, Mawasiliano kwa Umma na Uenezi.
Simu: 0653619906
Baruapepe: adoado75@hotmail.com

No comments:

Post a Comment