Pages

Pages

Pages

Saturday 5 March 2016

TFF YAZIKIMBIZA YANGA, SIMBA KOMBE LA SHIRIKISHO!

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) leo limetoa ratiba ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho ambayo brotherdanny.com inaona dhahiri kwamba shirikisho hilo limezikimbiza Simba na Yanga ili zisikutane mapema.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Simba na Yanga zinaweza zikakutana fainali endapo zitafuzu hatua hiyo ya robo fainali.
Badala yake, uwezekano uliopo ni kwa Azam kukutana na Simba kwenye nusu fainali ikiwa timu hizo zitavuka hatua ya sasa.
Ratiba kamili inaonyesha kwamba, Azam watacheza na Tanzania Prisons wakati Simba watavaana na 'Wagosi wa Kaya' Coastal Union kwenye robo fainali.
Aidha, Yanga itacheza na Ndanda FC wakati Geita Goldmine itacheza na Mwadui.
Brotherdanny.com inatambua kwamba, mchezo baina ya Simba na Yanga huwa unavuta hisia za mashabiki wengi na endapo timu hizo zitafanikiwa kufika fainali, itakuwa ni mechi kubwa iliyojaa visasi kutokana na Simba kufungwa mfululizo kwenye Ligi Kuu.

No comments:

Post a Comment