Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kushoto) akizungumza
na Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Virginia Blasser (katikati) pamoja na Kaimu
Naibu Balozi wa Marekani, Vicent D’Spera, kuhusu masuala mbalimbali ya
ushirikiano kati ya Wizara yake na Ofisi ya Kaimu Balozi huyo nchini. Viongozi
hao wa Ubalozi wa Marekani nchini walimtembelea Naibu Waziri Masauni ofisini
kwake jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kaimu Balozi
wa Marekani nchini, Virginia Blasser (kulia) akimfafanulia jambo Naibu Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni wakati Kaimu Balozi huyo
alipomtembelea Naibu Waziri Masauni ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo,
kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Ubalozi wa Marekani na Wizara.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kushoto) akifurahi jambo
na Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Virginia Blasser (katikati) pamoja na Kaimu
Naibu Balozi wa Marekani, Vicent D’Spera, baada ya kumaliza mazungumzo yao kuhusu
masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara na Ofisi ya Kaimu Balozi huyo
nchini. Viongozi hao wa Ubalozi wa Marekani nchini walimtembelea Naibu Waziri
Masauni ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
*****************************************************************************
No comments:
Post a Comment