Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari akiongea na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam leo, wakati alipofanya nao mkutano kwa mara ya kwanza tanga ateuliwe kushika wadhifa huo. Kushoto ni Mwanasheria wa TCAA, Patrice Chegani.
Baadhi ya wafanyaakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA, wakimsikilaza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo , Hamza Johari hayupo pichani, wakati alipokutana nao kwa mazungumuo ya utendaji kazi leo jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi wetu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw.Hamza Johari, amewataka wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kujiangalia pale wanapoona waliteleza na kubadilika kwa kufanya mabadiliko na kuachana na tamaduni walizoziea hapo awali.
Mkurugenzi Johari aliyasema hayo leo alipokuwa katika kikao chake cha kwanza kilichafanyikia TCAA Makao Makuu na kuhusisha wafanyakazi wa TCAA wa Makao makuu, kituo cha uwanja wa ndege wa JNIA, chuo cha usafiri wa Anga (CATC) na Karakana ya TCAA Chang’ombe baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni, na kuongeza kuwa kila mtu au kila jamii ina utamaduni fulani, tatizo ni tafsiri au namna tamaduni hiyo ilivyo inaweza kuwa nzuri ama mbaya.
Bw. Johari ameongeza pia kuwa yeye anawaona wafanyakazi wote wa TCAA kama timu moja ya ushindi na anaamini kwa kufanya kazi kwa kushirikiana basi TCAA itapiga hatua na ikitokea kinyume chake TCAA Itakwama .
Bw.Hamza pia amesisitiza juu ya kila mmoja kutimiza wajibu wake mahala pake pa kazi na yeye pia kama Mkurugenzi Mkuu atatimiza ya upande wake, lengo likiwa kuipigisha TCAA hatua.
Ameongeza pia kuwa, katika kipindi hiki cha uongozi wake atahakikisha masuala mbali mbali ambayo ni changamoto kwa wafanyakazi wa TCAA yanaangaliwa upya na kuboreshwa, ili waweze kuongeza Ari ya kufanya kazi.
Akitoa salamu ya shukran kwa niaba ya wafanyakazi wa TCAA, Katibu Mkuu wa TUGHE –TCAA Bw.Maotola Miti alimuakikishia Mkurugenzi Johari kwamba wafanyakazi wote wa TCAA wapo nyuma yake katika kufanikisha malengo ya TCAA kupiga hatua yanafanikiwa, na kuongeza kuwa wafanyakazi wa TCAA wana matumaini makubwa juu yake.
No comments:
Post a Comment