Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 8 March 2016

MKONO MMOJA WAIWEKA JUU YANGA, YAIKUNG'UTA AFRICAN SPORTS MARA 5 BILA MAJIBU


MABAO mawili ya Amissi Tambwe na mengine matatu yaliyofungwa na Kelvin Yondani, Donald Ngoma na Anthony Simon Matheo yalitosha kuirejesha Yanga kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom kwa ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya African Sports ya Tanga, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Kwa ushindi huo, Simba waliokuwa wanaongoza, sasa wamekaa kilele kwa saa 48 kabla ya kuwapisha tena Yanga, ambao sasa wanakwenda Rwanda Jumatano kucheza na APR katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika wakiwa na ari kubwa.
Yanga imefikisha pointi 50 wakati Simba ina pointi 48 ikifuatiwa na Azam ambayo ina pointi 47.
Lakini mshambuliaji Amissi Tambwe amefanikiwa kumpita Hamisi Kiiza wa Simba kwa idadi ya mabao ya kufungwa baada ya kufikisha mabao 17. Kiiza ana mabao 16.
Idadi aliyoifikia Tambwe kwenye ligi hiyo ni sawa na ile ya Simon Msuva wa Yanga, ambaye msimu uliopita aliibuka kinara wa ufungaji.
Hali hiyo inaonyesha dalili kwamba, ikiwa ataendelea kupangwa na hatapata majeraha, Tambwe anaweza kuongeza mabao mengine na kuibuka kinara wa ufungaji.
Msuva alifunga mabao hayo 17 na kuchukua kiatu cha Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara huku, Tambwe aliyekuwa ametokea Simba akiwa na bao moja akimaliza msimu akiwa na mabao 14 katika nafasi ya pili. Kabla msimu mmoja akiwa Simba, alikuwa ndiye mfungaji bora baada ya kupachika mabao 19.

No comments:

Post a Comment