Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 1 March 2016

MAKAMU WA RAIS MSTAAFU DKT. BILAL AKABIDHI ZAWADI ZA WASHINDI WA MASHINDANO YA KUTAFUTA WAWAKILISHI WA NCHI KATIKA MASHINDANO YA KIMATAIFA YA QUR'AN TUKUFU.

Makamu wa Rais mstaafu  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur'aan Tukufu, yaliyoandaliwa na Kamati Maalum chini ya Mwenyekiti wake Saleh Omary, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, Feb 28, 2016. Picha na Mafoto Blog.

Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu, waliohudhuria mashindano hayo, wakimsikiliza Dkt. Bilal, wakati akihutubia. Picha na Mafoto Blog.
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa kwanza wa Mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur'aan Tukufu, Rajai Ayoub, aliyepata pointi 95 kwa upande wa Tajweed, wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, Feb 28, 2016. Mashindano hayo yameandaliwa na Kamati maalum chini ya Mwenyekiti wake, Saleh Omary. Kushoto ni Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mahd Aghajafar . Picha na Mafoto Blog.
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mahd Aghajafar, wakati wa Mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur'aan Tukufu hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, Feb 28, 2016. Mashindano hayo yameandaliwa na Kamati maalum chini ya Mwenyekiti wake, Saleh Omary. Kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Al-had Mussa Salum. Picha na Mafoto Blog.
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa pili wa Mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur'aan Tukufu, Ibrahim Omary, aliyepata pointi 90 kwa upande wa Tajweed, wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, Feb 28, 2016. Mashindano hayo yameandaliwa na Kamati maalum chini ya Mwenyekiti wake, Saleh Omary. Kushoto ni Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mahd Aghajafar. Picha na Mafoto Blog.
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wakati akiondoka kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, baada ya kumalizika kwa mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur'aan Tukufu. Picha na Mafoto Blog.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sl-had Mussa Salum, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, kufunga mashindano hayo. Picha na Mafoto Blog.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mashindano hayo, Saleh Omary, akizungumza wakati wa mashindano hayo. Picha na Mafoto Blog.

No comments:

Post a Comment