Kocha mkuu wa Mbeya City Fc , Kinnah Phiri amesibitisha kuwa mlinda mlango mahiri wa kikosi chake Juma Kaseja hatakuwa sehemu ya nyota watakaoiwakililisha City kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara dhidi ya Simba Sports alub uliopangwa kuchezwa jumapili hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.
Muda mfupi uliopita kocha Phiri ameudokeza mtandao huu kuwa ilikuwa waungane na kipa huyo leo asubuhi kwenye kambi ya muda hapa Morogoro lakini imemlazimu kumuongezea muda zaidi wa kukaa karibu na familia yake ili kushughulikia masuala kadhaa ya kifamilia aliyonayo hivi sasa.
“Wakati anaondoka Mbeya siku tano zilizopita tulikubaliana kuwa ataungana nasi hapa siku ya leo, nimezungumza nae leo asubuhi kuna mambo muhimu ya kifamilia amenieleza hivyo basi nimeamua kumuongezea siku kadhaa za kubaki nyumbani kushughulikia yale yote yaliyopo kwenye familia yake na imani yangu kuwa ataungana na kikosi mara tu tutakaporejea mbeya kujiandaa na mchezo dhidi ya Stand United March 10.
Juma Kaseja aliondoka jijini Mbeya mara baada ya mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Tanzania Prison uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine kufuatia taarifa njema ya mkewe kujifungua watoto mapacha.
Wachezaji wanzeke na uongozi wa City kwa ujumla unampongeza Juma Kaseja na kumtakia kila la kheri kwenye malezi ya watoto wake.
No comments:
Post a Comment