Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akijitambulisha kwa
wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kabla
ya Kamati hiyo kuipokea taarifa ya Wizara hiyo katika kikao cha kwanza cha Kamati
hiyo baada ya kuundwa na Bunge hivi karibuni. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa
Kamati hiyo, Balozi Adadi Mohamed Rajabu anayefuatia ni Makamu wake, Kanali
Masoud Khamis. Kulia kwa Masauni ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali
Projest Rwegasira. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Kisenga jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi
Mohamed Rajabu akizungumza jambo na Wajumbe wa Kamati yake pamoja na Watendaji
Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kikao chao kwanza tangu Kamati
hiyo iundwe na Bunge hivi karibuni. Wapili
kulia mstari wa mbele ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad
Masauni, na kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest
Rwegasira. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Kanali Masoud Khamis. Kikao
hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kisenga jijini Dar
es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akitoa taarifa ya Wizara
katika kikao cha kwanza cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
Kikao hicho kilichohudhuriwa na Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Maafisa wa
Wizara, kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kisenga jijini
Dar es Salaam leo. Kulia ni Mwenyekiti
wa Kamati hiyo, Balozi Adadi Mohamed Rajabu. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Baadhi
ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,
pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni (hayupo
pichani) alipokuwa anawasilisha taarifa ya Wizara kwa Kamati hiyo katika kikao
kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kisenga jijini Dar es
Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (katikati) akiwa na
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira wakiiweka sawa
taarifa ya wizara yao kabla ya kuiwasilisha kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Balozi Adadi Mohamed Rajabu. Wajumbe wa Kamati
hiyo pamoja na Watendaji wa Wizara walikutana katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Kisenga jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kujadili masuala
mbalimbali ya Ulinzi na Usalama. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
********************************************************
No comments:
Post a Comment