Pages

Pages

Pages

Friday 12 February 2016

HATARI: MWANAMUME MZEE ANAWEZA KUZAA WATOTO WENYE MATATIZO YA KIMAUMBILE

Mbegu za kiume
Uzalishaji wa mbegu za kiume katika korodani ya mwanadamu wakati anapokuwa mzee huongeza hatari ya watoto wenye matatizo ya kimaumbile.
Mamilioni ya seli zinazotolewa wakati wa uzalishaji wa mbegu hizo hutoa mbegu nyingi za kiume katika korodani.
Lakini utafiti huo wa chuo kikuu cha Oxford nchini Uingereza unaonyesha kwamba mbegu hizo humea uvimbe na kusababisha mbegu nyingi za kiume kuwa na kasoro.
Wataalam wamesema kuwa wanandoa wanapaswa kupata watoto mapema katika maisha yao.
Magonjwa kadhaa ikiwemo ugonjwa wa akili wa watoto pamoja na dhiki hutokea sana miongoni mwa akina baba walio na umri mkubwa kutokana na Uzalishaji wa mbegu za kiume zilizo na kasoro.

Image copyrightSPL
Image captionMbegu za kiume

Na hatari kuu ya ugonjwa huo huwaathiri watoto wanne kati ya 200 hadi watano kati ya 200 kwa pamoja wakati baba anapopitisha umri wa miaka 50.
Utafiti huo, uliochapishwa katika chuo cha kitaifa cha sayansi, ulichunguza korodani 14 kutoka kwa wanaume walio kati ya umri wa miaka 39 hadi 90.
Viungo hivyo vilikuwa havina matatizo ya kiafya lakini viliondolewa kwa matatizo mengine.
Watafiti walichunguza ndani ya korodani hizo ili kujua ni maeneo yapi yanayotoa mbegu hizo za kiume.
Wachanganuzi wa DNA katika maeneo hayo yenye kasoro walibaini kwamba kuna uzalishaji wa mbegu zilizo na kasoro zilizosababishwa taratibu mbalimbali mwilini.
Zilihusishwa na saratani, lakini pia zilikuwa na jukumu la ukuaji na uzazi katika korodani.
Matatizo hayo ambayo huathiri watoto husababisha uzalishaji wa mbegu zaidi ambazo huenea na hivyobasi kusababisha kiasi kikubwa cha mbegu zilizo na kasoro.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment