Pages

Pages

Pages

Friday 22 January 2016

SHAABAN KISSU AMPONGEZA MSAMA

Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo akisisitiza jambo akiwa na DC wa Kondoa, Shaaban Kissu (kushoto) na Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama.

Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Wilaya ya Kondoa Shabani Kissu ampongeza Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama tamasha lake linajali na kuwasaidia wenye shida bila kuchagua dini.
Kwa mujibu wa Kissu mapato ya tamasha hilo yanasaidia wenye uhitaji maalum kama yatima, walemavu na wajane bila kujali dini wala kabila.
Kissu alisema Msama hutimiza matakwa ya jamii kupitia mapato yanayotokana na michango inayotokana na viingilio.
"Msama ni mfano wa kuigwa kwa sababu nguvu zake zote ni kwenye matatizo ya jamii ni mtu ambaye anaguswa kwa karibu na jamii, "alisema Kissu na kuongeza.
"Msama hajifirii mwenyewe bali hufikira kundi kubwa la jamii ambalo lina uhitaji maalum."
Kissu alisema kilichomgusa mapato yake yanayopatikana hachagui na tamasha limekuwa ni mkombozi wa watanzania wote.

No comments:

Post a Comment