Pages

Pages

Pages

Wednesday 9 December 2015

TAMISEMI YAENDELEA KUHAMASISHA SUALA LA USAFI JIJINI DAR

 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba (aliyevaa miwani) akishuhudia Majuto Alli Majuto akiendelea na kazi yake ya kukaanga samaki aina ya pweza katika soko la samaki la Feri jijini Dar es salaam.


 Vijana wakiendelea kazi ya kukaanga samaki katika soko la Feri katika mazingira ambayo hali ya usafi siyo ya kuridhisha kwa ajili ya kulinda afya ya mlaji.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Dar es salaam na Halmashauri ya Wilaya ya Ilala wakiwasili eneo la soko la Feri jijini Dar es salaa kujionea hali ya usafi wa soko hilo.

Baadhi ya wahudumu wakiendelea na usafi eneo la soko la Feri jijini Dar es salaa huku Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba na msafara wake wakikagua na kujionea hali ya usafi wa soko hilo.

 Kijana Hamisi Misango akimnyanyua samaki aina ya taa ili amuandae tayari kwa kumuuza kwa wateja wanafuata kitoweo katika soko la samaki la Feri jijini Dar es salaam.
 Msafara wa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba wakishuhudia moja ya shimo la maji mchafu ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wa afya ya wananchi wanaofika katika soko la samaki la Feri jijini Dar es salaam au wale watakaotumia samaki hao kama hawatakuwa wameandaliwa katika hali ya usafi na salama. Lengo ni wananchi wengi wanaofika sokoni hapo ni kununua samaki waweze kuwauzia watu wasoweza kufika sokoni hapo na wengine kwa ajili ya matumizi yao ya nyumbani.
 
 Mama lishe Zainabu Hamad anayefanya shughuli zake za kutoa huduma ya chakula katika soko la Feri zoni 4 kizimba namba 12 akiongea na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba alipotembelea sokoni hapo kwa lengo la kuhamasisha suala la usafi kwa manufaa ya kulinda afya ya wananchi wanatumia huduma hiyo wakiwa sokoni humo.
Biashara mbalimbali ikiwemo ya kijana aliyekuwa akiuza mayai zikiendelea katika eneo la soko la Feri jijini Dar es salaam bila ya kuzingatia kanuni za afya na hatari iliyopo ya magonjwa wa mlipuko ikiwemo kipindupindu.
 Mfanyabiashara wa Soko la Kariakoo Mwajabu Mdeme akimueleza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba kero zinazowasumbua sokoni hapo ikiwemo huduma mbovu ya maji, maji machafu kutapakaa sehemu mbalimbali, huduma duni ya choo na joto kali eneo la Shimoni.
 Baadhi ya maeneo yaliyokithiri kwa uchafu katika soko la Kariakoo.
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba na msafara wake wakiwa katika eneo la soko la Kariakaoo kukagua suala la usafi unavyozingatiwa sokoni humo. Licha ya uchafu uliopo katika soko la Kariakoo, wafanyabiashara wa matunda hawachukui tahadhari yeyote ya kulinda afya za walaji wa matunda ambapo wanauza matunda aina ya mananasi bila kuyafunika sa kusababisha inzi kuyazonga zonga matunda hayo kitu ambacho ni hatari kwa suala la usalama wa afya ya malaji.
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba akijionea wafanyabiashara wadogo walivyovamia miundombinu ya Mradi wa Mabasi yaendayo kwa kasi katika eneo la Kariakoo jijini Dar es salaam huku mafundi wakiendelea na kazi ya kupaka rangi.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba akitembelea maeneo mbalimbali ya soko la Kariakoo jijini Dar esa salaam.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

No comments:

Post a Comment