Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 6 October 2015

WIZARA YA UJENZI YAELEZEA MAFANIKIO YAKE KWA KIPINDI CHA MIAKA 10


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Ujenzi, Segolena Francis (kulia), akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo asubuhi wakati akimkaribisha Mkurugenzi wa Barabara wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Ven Ndyamkama (kushoto), kuzungumza na waandishi wa habari  kuhusu mafanikio ya serikali katika sekta ya ujenzi kwa kipindi cha  miaka 10 kuanzia mwaka 2005 hadi 2015.


Mkurugenzi wa Barabara wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Ven Ndyamkama (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, kuhusu mafanikio ya serikali katika sekta ya ujenzi kwa kipindi cha  miaka 10 kuanzia mwaka 2005 hadi 2015. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa wizara hiyo, Segolena Francis.
Hapa mkutano ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

WIZARA ya Ujenzi imesema itashirikiana na Sekta Binafsi (PPP) kuhakikisha kuwa baadhi ya miradi ya barabara inajengwa na sekta hiyo ili kukamilisha miundombinu ya usafiri nchini.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Barabara katika Wizara hiyo Mhandisi Ven Ndyamukama wakati akizungumza na waandishi wa habari leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam.

Alisema mfano wa mradi wa ushirikiano wa Serikali na PPP ni barabara ya Dar es Salaam hadi Chalinze ambayo itakuwa na njia sita unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Alisema lengo la Serikali kushirikiana na sekta binafsi ni kuhakikisha kuwa miradi mingi inakamilika kwa wakati ambapo kwa kipindi cha miaka 10 ya Serikali ya awamu ya nne wamekamilisha ujenzi wa kilometa 5,568 za lami zilizogharimu sh. bilioni 4,090 kati kilometa 17,762 ambazo zilitarajiwa kujengwa.

"Tumejipanga kushirikiana na sekta binafsi katika utekelezaji wa miradi mingi hapa nchini lakini kwa kuanza ni huu wa Dar es Salaam hadi Chalinze unaotarajiwa kuanza hivi karibuni," alisema.


Pia alisema kilometa 3,873 zinaendelea kujengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya jumla ya sh.bilioni 4,533 na barabara zenye urefu wa kilometa 4,965 zimefanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa gharama ya shilingi bilioni 29.257 ambapo Serikali inatafuta fedha za ujenzi wa lami.

No comments:

Post a Comment