Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene( katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Ileje Rosemary Senyamule kulia wakifurahi jambo katika sherehe hizo . |
Sherehe zikiendelea |
Na Jamiimojablog.
Naibu Waziri wa Viwanda an Biashara Janeth
Mbene amezindua siku ya mwanamke wa
Ileje ambayo imeanza kuazimishwa Oktoba mosi kwa kuwakutanisha wanawake kutoka
katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kubadilishana uzoefu.
Pia maadhimisho hayo yanalenga kujifunza masuala mbalimbali yakiwemo ya Afya,
na Uchumi ili kujikomboa kutoka kuwa
tegemezi an kujitegemea kwa kipato.
Katika
ufunguzi wake Mbene amewataka Wanawake wilayani humo kutuitumia vyema siku hiyo
kwa kuha kikisha wana jadili changamoto zinazowakabili ili waweze kujikwamua
kiuchumi kutoka walipo na kuwa katika hali nzuri kimaisha.
Mbene amewataka wanawake ambao ni
nguzo ya familia kuziangalia changamoto walizonazo, ambazo alisema kila
changamoto iliyopo wahesabu kama inawaathiri mara mbili (ni dozi mara mbili)
hivyo lazima wao wenyewe wawe tayari kuzikataa kwa kushirikiana an wengine.
Amesema zipo fursa nyingi katika
wilayani humo ambazo kama zinatumia vizuri zitaweza kuwanufa akina mama hao
hivyo ni wakati wao kuzitumia fursa hizo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Mbene ambaye pia ni mgombea ubunge
kwa tiketi cha Chama cha mapinduzi (CCM)katika jimbo la Ileje amesema moja ya
fursa ambayo kama itatumia vizuri
ianweza kuwainua akina mama hao ni pamoja na kuanzisha vikundi mbalimbali
vitakavyo jihusisha na shughuli za kilimo cha mbogamboga.
No comments:
Post a Comment