Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Tuesday, 6 October 2015
MAJENGO YA MKANDARASI KUGEUZWA CHUO CHA UFUNDI VETA
Na Mwandishi Wetu, NzegaMGOMBEA Ubunge kwa tiketi CCM jimbo la Nzega Mjini Hussein Mohamed Bashe amesema akichaguliwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha majengo ya kampuni ya Chinese Construction Company Limited (CCC) ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Nzega hadi Puge yanakuwa chuo cha ufundi stadi Veta.
Bashe akiwahutubia wananchi wa mtaa wa majengo alisema kutokana na vijana wengi kushindwa kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali majengo hayo yatageuzwa matumizi kuwa chuo cha Veta kitakachoweza kusaidia vijana ambao wangeweza kujiunga na makundi ya uhalifu.
Bashe alisema kuwa fursa hiyo itatokana baada ya wananchi kumchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo la Nzega mjini iliaweze kuwatumikia wananchi.
Alisema kuwa Mgombea Urais wa chama hicho John Magufuli alimwambia wakati alipopita katika ziara yake na kupewa ahadi ya suala hilo kuwa endapo atakuwa rais wa jamuhuri ya muungano ambi hilo litafanyiwa kazi na wananchi kunufaika na majengo hayo kwa kupata chuo cha VETA.
Alisema katika sula la kupata chuo cha VETA anakila sababu ya kufanya jitihada kutokana na kundi kubwa la vijana kukosa ajira na badala yake kujikita katika matumizi ya madawa ya kulevya hali ambayo ni madhara kwa afya zao na familia kwa ujumla.
Kwa upande wake mgombea udiwani wa kata ya Nzega mashariki Elface Luangisa alisema changamoto mbalimbali za kata hiyo anazifamu ikiwa na ukosefu wa kituo cha afya ambapo kwa sasa wananchi hupata shida kupata huduma za afya katika eneo hilo.
Aliwataka ilikupata maendeleo ya uhakika bila matatizo wananchi wanapaswa kuchagua mbunge wa ccm,diwani wa ccm pamoja na rais.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment