Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 1 October 2015

KATI YA OBAMA NA ZUMA NANI ALIKOSA HESHIMA?

Rais Barack Obama wa Marekani akimsalimia Jacob Zuma wa Afrika Kusini huku akimuugilizia kama anaongea na simu.
Je ukimpata mtu anazungumza kwa simu utamuamkua ama utamsubiri akamilishe mazungumzo yake kisha umpe salamu zako ?
Hilo ndilo swali kuu lililoibuka kwenye mkutano wa viongozi duniani katika makao makuu ya umoja wa mataifa huko New York Marekani.
Rais wa Marekani Barack Obama alimpata rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akizungumza kwa simu.
Rais Obama akasisitiza kumuamkua na kwa sababu moja au zaidi rais Zuma hakukata simu yake aliendelea kuzungumza na kumuacha Obama ameduwaa.
Mpiga picha mmoja alipata picha hiyo na kuiweka kwenye mtandao wa kijamii.
Image captionJe Obama alipaswa kusibiri rais Zuma akamilishe mazungumzo yake kwa sababu anamzidi umri ?
Picha hiyo imekuwa maarufu sana haswaa Afrika Kusini ambapo watu wengi wanasema kuwa Obama hakuwa na adabu hata kidogo.
kwa mujibu ya wa waliochangia kwenye mitandao ya kijamii Obama alipaswa kusibiri rais Zuma akamilishe mazungumzo yake kwa sababu anamzidi umri.
Mjadala huo umechacha hususan baada ya gazeti la Times Live kuwauliza wasomaji wake watoe maoni yao.
Je unakubaliana nao kuwa Obama alipaswa kumsubiri Zuma akamilishe mazungumzo yake
Toa maoni yako kwenye mtandao wetu wa Facebook na Twitter tafuta BBCSwahili?
BBC

No comments:

Post a Comment