Pichani Ndugu Saidi Mwamende akimuliza swali Mhe: Jussa, (Hayupo Pichani)
Na Swahilivilla. Blog Washington
Waziri Majivuno wa Kusadikika alisema: "Hekima ni kitu adimu kupatikana kwa mtu asiye na mvi...". Pia Waswahili wanasema: "Akili ni nywele"
Mhe: Ismail Jussa akijibu swali la Saidi Mwamende (Hayupo pichani)
Katika mkutano huo uliofanyika tarehe 28 Februari mwaka huu jijjini Washington, Bwana Ismail Jussa, aliwathibitishia Wanadiaspora wa Tanzania nchini Marekani pamoja na ulimwengu kwa ujumla kuwa Elimu ilipokuwa haijulikani hapa duniani, mvi zilizingatiwa kuwa ni ishara ya hekima, lakini nadharia hiyo wakati wake umepita na hautorejea tena. Kwani katika kujibu swali la Katibu wa Jumuiya ya Watanzania kwaishio jijini Washington na vitongoji vyake Bwana Said Mwamende, Mheshimiwa Jussa alisema ni mapema mno kulitolea kauli swala hilo, ispokuwa "nitasema moja ambalo litatosheleza swali lako"
'Moja' hilo la Mwakilishi huyo wa Jimbo la Mji Mkongwe, Zanzibar ambaye nywele zake bado ni nyeusi, linathibitisha kuwa nafasi hiyo aliyonayo kupitia ridhaa ya wananchi wa Jimbo lake hakuipata kwa sudfa tu, bali alistahiki na anaistahiki. Bali ni Mwanasiasa aliyekomaa na mwenye kuona mbali. "Nilisema mapema kwamba nazungumza na Mwenyekiti Mbowe, nazungumza na Mwenyekiti Lipumba na nazungumza na Mwenyekiti Mbatia. Sioni kwamba kwa wote hao kuna fikra ya ung'ang'anizi kwamba lazima niwe mimi". Alisema Bwana Jussa kwa kujiamni, na kusisitiza "Hilo silioni kwa sasa hivi". Upana wa wigo wa mawasiliano yake hayo unadhihirisha ukomavu wa akili yake, na kwamba fikra zake hazikufungika ndani ya vichochoro vya Mji Mkongwe, bali zimevuka Bahari ya Hindi na kuangaza Tanzania yote na hata nje ya mipaka yake. Mheshimiwa Jussa hakuwa anastawisha Baraza tu au 'kumwondosha njiani' Bwana Mwamende, bali alikuwa anazungumzia uhalisia wa mambo yanavyopaswa kuwa. Aidha hakuwa akitumia ulaghai wa kisiasa pale aliposema: "Na ninachojua ni kwamba viongozi wetu wanaangalia hata nje ya vyama katika kupata mgombea ambaye ataweza kuwakilisha vyema misimamo na ajenda ambayo UKAWA inaisimamia". Bwana Jussa ambaye kitaaluma ni msoni wa Sheria, alidhihirisha wazi kipaji chake cha kuweza kushtukia na kufichua mbinu sa kisiasa zilizojificha. Aidha si mtu anayekhofu kuelezea maoni yake binafsi kwa manufaa ya umma. Haya yanaonekana alipoendelea kunena: "Nikwambie kitu kimoja, hili ni mawazo yangu binafsi: 'Mimi nahisi CCM wana khofu na hilo unalolisema kama Chama. Na ndiyo maana tulikuwa tunajua sote kwamba CCM ilikwisha tangaza kwamba Mkutano wao Mkuu wa kumpata mgombea ulikuwa umepangwa kufanyika mwezi wa April. Lakini juzi tulimsikia Nape Nnauye akisema kuwa kutokana na sababu ya kura ya maoni, na Bunge la Bajeti linofuata baadaye, itakuwa vinaingiliana. Kwa hivyo bora uakhirishwe mpaka baada ya Bunge la Bajeti'.." Kigogo huyo wa Chama Cha Wananchi CUF, aliitafsiri kauli hiyo ya CCM kama ni mbinu ya kuvuta wakati na kwenda karibu na uchaguzi wakidhani wataweza kuliepuka jambo hilo. "Kwa hiyo, tafsiri yangu ni kwamba wanataka kwenda zaidi, ili wakidhani wataweza kuliepusha hilo" Alichambua bwana Jussa ambaye kadiri nywele zake zinavyopotea, ndivyo akili zake zinavyozidi kukomaa.
Pichani Makamu Mwenyekiti wa CUF wakati huo, Maalim Seif Sharif Hamad (kulia) na Mwakilishi wa sasa wa Mji Mkongwe, Ismail Jussa.
Tangu ujanani mwake, Mheshimiwa Ismail Jussa alikuwa akipenda kukaa na watu wazima akijua kuwa huko ndiko kwenye hazina za hekima na maarifa. Mwenendo wake huo, ndio uliopanua muono wake na kuweza kuichambua CCM na kuielezea kuwa ni Chama kilichopoteza mwelekeo, itikadi na misingi kiliyoasisiwa chini yake, na kwamba kilichobaki ni makundi makundi ndani yake yenye kupigania maslahi binafsi.
"Kwa jinsi ninavyoona, ile CCM ya Nyerere ambayo mpo pale kwa sababu ya Ujamaa na Azimio la Arusha haipo tena. Kilichobakia ni kwamba ni vipi kila mtu na kundi lake na rafiki zake watafanikiwa kupata nafasi wakavuruge nchi"
Jussa si mtu wa papara wala pupa, bali mtu ni mwenye subira, na alimtaka Bwana Mwamende kujiunga naye katika mbuga ya subira na kuupa nafasi wakati ufanye kazi yake.
"Kwa hiyo ninachosema, hayo tuyaachie wakati wake ukifika. Kama atatoka miongoni mwa hao, kama atatoka nje ya hao, au kama atatoka miongoni mwa viongozi wa UKAWA tuuachie wakati utasema".
Aidha kwa mara nyengine alisisitza imani yake juu ya viongozi wa Vyama vinavyounda UKAWA juu ya msimamo wao wa kuwa na mgombea mmoja:
Nataka nikuhakikishie kuwa kwa upande wa UKAWA si hoja kwamba awe Lipumba, Slaa, Mbowe au Mbatia. Si hoja kabisa kwa sasa hivi. Hoja ni nani ataweza kubeba bendera ya UKAWA"
Mheshimiwa Jussa alimalizia jibu lake kwa kusema "Nadhani tutafika vizuri".
Kauli hiyo ilikuwa inatabiria "Safari ya Matumaini" ya Mheshimiwa Edward Lowassa iliyogeuka na kuwa "Safari ya Uhakika".
Naam, akili si nywele, na wala mvi si dalili ya hekima. Bali elimu ndiyo mwangaza, khaswa pale inapotiliwa nguvu na tabia ya kukaa na watu wenye busara. Maneno aliyoyasema Mheshimiwa Jussa tarehe 28 Februari 2015 nchini Marekani, ndiyo ambayo leo hii yanatuongozea siasa za Tanzania.
No comments:
Post a Comment