Msanii wa nyimbo za Injili raia wa Uingereza, Ifheanyi Kelechi (katikati) ,
akiwasili leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini
Dar es Salaam, tayari kutumbuiza katika Tamasha la Amani linalofanyika leo
Uwanja wa Taifa Dar. Kulia ni Mkurugenzi wa Msama Promotions wanaoratibu
tamasha hilo, Alex Msama. Kushoto ni Mratibu, Hudson Kamoga. (Picha na Francis
Dande)
NA
MWANDISHI WETU
RAIS
Jakaya Kikwete kesho Jumapili Oktoba 4 anatarajiwa kuwaongoza maelfu ya watanzania katika Tamasha
la kuombea amani Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, linalofanyika katika Uwanja wa
Taifa, jijini Dar es Salaam
chini ya uratibu wa kampuni ya Msama Promotions.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam
jana, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama alisema maandalizi yote
yamekamilika ikiwemo kuwasili kwa waimbaji wa kimataifa Sipho Makhabane na
Solly Mahlangu kutoka Afrika Kusini na Ifeanyi Kelechi kutoka nchini Uingereza.
Alisema
waimbaji hao nguli wa muziki wa injili Afrika, wamekuja kuungana na wengine
mahiri wa hapa nchini kupamba Tamsha hilo la kihistoria litakalohudhuriwa na
viongozi wa kiroho wa ndani na nje ya nchi wakiwamo wachungaji zaidi ya 200 na
maaskofu 50.
“Hili
ni tukio la aina yake kwani tunaingia katika kipindi kigumu cha uchaguzi mkuu
unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa pengine kuliko yote iliyopita, hivyo tuna
kila sababu ya kumtanguliza Mwenyezi Mungu, tuweze kuvuka salama,” alisema
Msama.
Alisema
lengo la kuandaa Tamasha hilo ni kutokana na kutambua umuhimu wa tunu ya amani
kwa ustawi wa nchi iwe kijamii hata kiuchumi na kuongeza kuwa amani iliyopo
inapaswa kulindwa na kila mmoja kwa nafasi yake.
Msama
alisema kwa vile Mungu ni wa wote bila kujali dini, jinsia wala kabila na
amekuwa akisikia maombi ya watu wake na kuyajibu, wananchi hawana budi
kujitokeza kwa wingi katika tamsha hilo kuomba
nchi ivuke salama katika uchaguzi huo wa Oktoba 25.
Kwa
upande wa buruidani, mbali ya Mahlangu na Makhabane kutoka Afrika Kusini,
waimbaji wengine wanaotarajiwa kupamba tamasha hilo
ni Ephraem Sekeleti kutoka Zambia ,
Sarah K kutoka Kenya na Solomon
Mukubwa, raia wa DR
Congo anayeishi nchini Kenya .
Waimbaji
wa Tanzania, ni Rose Muhando, Upendo Nkone, Jesca BM, Martha Mwaipaja, Christopher
Mwahangila, Bonny Mwaitege, John Lissu, Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama, St.
Andrew Anglican ya Dodoma na AIC Chang’ombe ya jijini Dar es Salaam.
Msama
alisema viingilio kwa viti maalumu ni shilingi 5,000, jukwaa kuu shilingi 3,000
kwa wakubwa na watoto watalipa shilingi 1,000 na kuongeza ameweka kiwango hicho
kutoa nafasi wengi kushuhudia na baada ya uwanja wa Taifa, litahamia katika
mikoa mingine.
Kwa
kutambua umuhimu wa amani kwa mustakabali wa taifa, Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), kimepongeza uwepo wa tamasha hilo na kusema litumike pia
kumwombea Rais Kikwete akubali kuyapokea matokeo ya aina yoyote yatakayoamuliwa
na wananchi kupitia sanduku la kura.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alisema
wanatoa angalizo hilo
kutokana na baadhi ya viongozi wa chama tawala (CCM) kwa nyakati tofauti kusema
hawatakubali kuachia upinzani Ikulu.
Mnyika
amesihi Tamasha hilo
litumike pia kuombea Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Chini ya Jaji Mstaafu,
Damian Lubuva, isimamie uchaguzi huo kwa mujibu wa sheria na taratibu ili uweze
kuwa wa huru na haki.
No comments:
Post a Comment