Pages

Pages

Pages

Tuesday 1 September 2015

WATAKIWA KUKATA LESENI ZA UCHIMBAJI MADINI

Wachimbaji wadogo wakiwa kwenye mkutano

Na Hastin Liumba, Nzega
OFISI  ya  Afisa  Madini   Mkazi  Tabora   imewataka   wafanyabiashara  wa madini Mgodi mdogo wa dhahabu  wa  Mwanshina  uliopo  wilayani Nzega  Mkoani  Tabora   kukata  Leseni za Biashara  hiyo ili waweze kuwa  na sifa  na kukidhi  mahitaji  ya sheria mpya ya madini  ya mwaka 2010.

Mgodi  huo una zaidi  ya wafanya Biashara  60  wa dhahabu  ambao hawana Leseni na hawatambuliki na wizara  ya Nishati na Madini  hali inayopelekea  serikali kuu  na wilaya  kushindwa  kukusanya  mapato ambayo yanegeweza  kutatua matatizo mbalimbali  ya kijamii.

Akizungumza na uongozi  wa mgodi huo Mtaalam  wa miamba  ya madini Joseph  Ngullumwa aliwataka viongozi hao kuhakikisha wafanya biashara wanao nunu dhahabu katika mgodi huo wasajiliwe na kutambulika na wizara ya madini ilikuweza kupata stahiki zao.

Alisema kitendo cha kukwepa  kusajiliwa na wizara ya madini ni kuisababishia hasara serikali  ya kutokusanya mapato ambayo yangeweza kutatua kero mbalimbali za wananchi.

Masumbuliko  Jumanne  meneja mkuu wa mgodi huo alisema jitihada mbalimbali zinaendelea kufanyika ili kuhakikisha wafanya Biashara wanapatiwa Elimu  ya kusajiliwa na kupata Leseni   ambayo itawasaidia kufanya kazi zao kwa uhuru  mkubwa tofauti na sasa wanafanya kazi kwa kificho.

Hata hivyo wafanya biashara hao hawakuweza kupatikana kwa muda huo na kuonogeza kuwa  zaoezi hilo litafanyiwa kazi na uongozi wa mgodi iliwapatikane na kusajiliwa haraka kama maagizo  ya  sheria mpya ya madini  ya mwaka 2010  inavyowataka  wafanya biashara hao.

Samweli  Nhindilo  katibu wa mgodi  huo  alisema   endapo wafanya biashara wataitikia  wito huo na kufuata masharti  ya serikali mgodi huo utakuwa umetimiza mmoja ya vigezo vikubwa  na kuweza kujua kiasi gani cha dhahabau kimepatikana kwa muda tangu uchimbaji ulipoanza.

Alisema serikali  ya wilaya na serikali  kuu zitapata mapato kupitia wafanya biashara hao endapo watakata  Leseni jamii itanufaika  kupitia mapato  hayo.

Hata  hivyo Ngassa  Gakune mtaalam  wa miamba  ya madini aliwatahadharisha viongozi  hao kuhakikisha usalama wa mashimo  ya wachimbaji ambayo  yanapaswa kukaguliwa kwa nyakati tofauti tofauti ili kuepuka ajali zisizo za lazima.

No comments:

Post a Comment