Pages

Pages

Pages

Saturday 26 September 2015

WALINDA AMANI WA AFRIKA KUSINI KUADHIBIWA

Monusco
Wanajeshi wa Afrika Kusini wadaiwa kuhatarisha usalama wa wanajeshi wengine
Wanajeshi hamsimi wa Afrika Kusini waliokuwa wakihudumu katika kikosi cha Umoja wa Mataifa kinacholinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Monusco) wameagizwa kurejea nyumbani.
Viongozi wa jeshi nchini Afrika Kusini wamesema wanajeshi hao wataadhibiwa kwa kuwa wamekiuka maadili ya utendakazi.
Taifa hilo lina takriban wanajeshi 1,400 wanaohudumu Congo, wakijaribu kusaidia kukomesha vita mashariki mwa DR Congo.
Baadhi ya wanajeshi wanadaiwa kuhatarisha usalama wa wanajeshi wengine wa UN nchini DR Congo.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment