Pages

Pages

Pages

Tuesday 29 September 2015

UKAWA, CCM KWENYE MCHUANO MKALI TABORA



Na Hastin Liumba, Tabora

UNAWEZA kwa sasa ukasema bila kumung`unya maneno kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 utaacha historia, lakini hata kwa majibo yaliyoko mkoani Tabora licha ya kuwa siku zote hutwaliwa na CCM safari hii lolote linaweza kutokea.
Unaweze ukasema kwa sasa wapiga kura wa leo siyo wale wa chaguzi zilizopita za mwaka 1995, 2000, 2005, 2010 na 2015 yawezekana wamebadilika au ni uzoefu wa kujifunza kupitia chaguzi zilizopita.
Kutokana na hilo niliamua kuzunguka majimbo yote 12 ya mkoa wa Tabora ili kujiridhisha na mchuano ulivyo kwa sasa kipindi hiki kampeni za lala salama.

Kuna majimbo yaliyoko mkoa wa Tabora kwa sasa baada kugawanywa  mapya ni majimbo mapya ya Nzega vijijini,Ulyankulu na Manonga.
Majimbo mengine ya zamani ni Nzega mjini, Bukene, Urambo, Kaliua, Sikonge, Igalula, Tabora Kaskazini, Igunga na Tabora mjini.
Kwa sasa majimbo haya tayari mtanange wa kampeni umepamba moto huku majimbo mengine hadi sasa hayajaa kampeni kutokana na sababu zisizoweza kufahamika.
Aidha kutokana na utafiti niliofanya nimegundua kuna majimbo kadhaa kwa sasa moto unawaka hasa kutokana nguvu ya UKAWA ilivyo kwa sasa.
Tuje jimbo la Kaliua ambalo UKAWA wamemsimamisha aliyekuwa mbunge wa viti maalumu (CUF) Magreth Sakaya ambaye kwa sasa anapambana na mbunge aliyetete jimbo kwenye kura za maoni Profesa Juma Kapuya.
Uchunguzi unaonyesha wawili hawa wanapamba vikali licha ya kuwepo kwa taarifa kuwa mzee Kapuya anaweza kuangukia pua kama hali ya sasa ya wananchi wa jimbo hilo wataendelea kuwa kama walivyo.
Hata hivyo kuna taarifa kuwa ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Kaliua wamegawanyika huku wengine wakimsapoti Iman ambaye inadaiwa eti matokeo yake yalichakachuliwa.
Taarifa za mtoa nyepesi anasema kuna kundi kubwa linamuunga mkono Iman hivyo kuna uwezekano usiopingika kuwa kundi hilo litaasi tu.
Tukija upande wa pili wa mgombea wa UKAWA kwa tiketi ya CUF Magreth Sakaya safari hii amejipanga vilivyo kwani hata akiwa mbunge viti maalumu katika bunge lililopita alikuwa akimsumbua sana jimboni humo.
Mama huyo hodari wa kuongea nje na ndani ya Bunge amekuwa hodari wa kuongea kutetea wanyonge hicho ni kitu ambacho kinampa nguvu na pengine hata akashinda kwa kishindo.
Duru za siasa jimboni humo zinasema wapiga kura wa jimbo hilo la Kaliua wamebadilika sana na wanatamka wazi kuwa wanampa Magreth Sakaya.
Aidha wengine wanasema kitu ambacho kilikuwa kinampa Profesa Juma Kapuya ni kura za jimbo jipya la Ulyankulu ambalo limetokana na jimbo la Kaliua.
Aidha kwa upande wa jimbo la Tabora Kaskazini jimbo hili mgombe wa CCM ni Almas Maige na UKAWA ni Joseph Kidaha ambaye huyu alikihama cha cha mapinduzi CCM na kujiunga na UKAWA akipinga matokeo ya kura za maoni.
Joseph Kidaha alishika nafasi ya tatu kura za maoni CCM na mpinzani wake Almas Maige yeye alishika nafasi ya kwanza huku mbunge aliyekuwa akitete jimbo hilo Shafin Sumar akiangkua.
Baadhi yawanaCCM jimboni humo wanasema mwenendo ulivyo mgombea wa UKAWA Joseph Kidaha anaweza kushinda kwani kuna kundi la wafuasi wa CCM hawakuridhishwa na mwenendo wa kura za maoni.
Huku wengine wakisema takrima ilikuwa ya dhahiri na rafu hapa na pale lakini zilifumbiwa macho.
Jimbo la Igalula yupo Musa Ntimizi ambaye ambaye alikuwa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Uyui,huyu anapambana na Mohammed Magozi ambaye kuna taarifa kuwa baadhi ya wafuasi wa aliyekuwa mbunge jimbo hilo Dk Athuma Mfutakamba.
Wafuasi wa mbunge huyo wa zamani imedaiwa wanapitapita baadhi ya kata kushawishi wapiga kura wapigie UKAWA kwani hawajaridhika na kura za maoni kwani mgombea wao alionewa.
Hapa sina hakika sana kama UKAWA wanaweza wakaambulia jimbo hilo bado nguvu ni ndogo.
Kwa upande jimbo Manonga mgombea wa CCM ni Seif Gulamali na UKAWA ni Issa Nguzo wanachuana vikali lakini CCM wana nafasi kubwa ya kushinda.
Jirani na jimbo hilo lipo la Igunga,ambapo mbunge wake Dk Dalali Kafumu alishinda kura za maoni lakini anapamba na mgombea wa UKAWA Mwigulu Daruweshi ambapo lolote linaweza kutokea hasa ikikumbukwa CCM walishinda kwa taabu jimbo hilo.
Ni ukweli usiopingika jimbo la Igunga UKAWA wana nafasi kubwa kwani wakazi wake wanaipenda CHADEMA zaidi kuliko CCM.
Aidha jimbo la Nzega mjini mgombea wa CCM Hussein Bashe ana nafasi kubwa ya kumshinda mpinzani wake kupitia UKAWA Charles Maguna kwani Bashe bado anakubalika sana.
Ikumbukwe Hussein Bashe alikuwa mfuasi mkubwa wa mgombea Urais kwa tiketi ya UKAWA Edward Lowassa maarufu kama mcheza sinema mwenye uwezo mkubwa katika filamu ya Don 2 (Feruzi).
Tukija katika jimbo la Nzega Vijijini yupo Dkt Hamis Kigwangalah kwa tiketi ya CCM akipambana na mgombea wa UKAWA Joseph Malongo lakini UKAWA inabidi wafanye kazi ya ziada kushinda.
Uchunguzi unaonyesha jimbo la Sikonge yupo George Kakunda huyo ni wa CCM akipambana na mgombea wa UKAWA Hijja Ramadhan Chambala ambaye alikuwa diwani wa Iplole kwa tiketi ya CHADEMA.
Chamballa ana uwezo mkubwa na ni msomi wa UDSM na alionyesha uwezo mkubwa katika baraza la madiwani lililopita kwa hoja zake.
Hata hivyo bado wawili hawa wako nusu kwa nusu kwani yoyote anaweza kushinda lakini kuna taarifa ndani ya CCM kunafukuta kutokana na kura za maoni.
Ndani ya CCM lipo kundi kubwa ambalo halikuridhishwa na matokea ya kura za maoni hasa baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Said Nkumba kuanguka.
Hali hiyo ilisababisha madiwani kadhaa wa kata za Mibono Mariam Ukongo kuhamia CHADEMA,Omari Kategile Sikonge Mjini kuhamia ACT-Wazalendo, Mashaka Msalangi Kipanga naye kuhamia CHADEMA.
Kata nyingine ambako wenda zikaenda UKAWA ni Kiloli, Kipili, Misheni, Kitunda kwenye machimbo ya Madini na Ipole ambayo awali ilikuwa chini ya CHADEMA.
Jimbo la Urambo kwa aliyekuwa spika wa Bunge Samweli Sitta safari kwa tiketi ya CCM amesimama mke wake Magreth Sitta ambaye anapambana na mgombea wa UKAWA Samweli Ntalamlanga wawili hawa wako nusu kwa nusu lolote linaweza kutokea.
Taarifa za uchunguzi zinaeleza majimbo ya Bukene mgombea wa CCM Suleiman Zedi anapambana na mgombea wa UKAWA Alex Simbi lakini UKAWA wanatakiwa kujipanga ili kushinda,Zedi ana nguvu bado huku Ulyankulu John Kadutu aliyekuwa mwenyekiti halmashauri ya Kaliua akichuana na Dkt Deus Kitapondya.
Jimbo hili UKAWA wajipange kwani John Kadutu ana nguvu licha ya wanaCCM 203 kuhamia CHADEMA lakini haitoshi kujihakikishia ushindi.
Aidha jimbo la Tabora mjini kuna mgombea wa CCM Emmanuel Mwakasaka na Yule wa UKAWA ni Peter Stewart Mkufya hawa wanachuana vikali.
Hata uchunguzi unaonyesha hata kama CCM itatetea majimbo kadhaa itakuwa ni kwa nguvu ya ziada kwani usaliti ndani ya chama hicho ni mkubwa japokuwa hata uwepo wa mabadiliko ndani ya jamiii kuhusu uchaguzi.
Mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA Edward Lowassa kushoto na yule wa CCM kulia John Magufuli.Picha na Hisan ya Mtandao


hastinliumba@gmail.com-0788390788

No comments:

Post a Comment