Pages

Pages

Pages

Friday 4 September 2015

RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA TAKWIMU HURIA KANDA YA AFRIKA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akifungua mkutano wa siku mbili wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika unaofanyika nchini katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Bella Bird (wa kwanza kulia).

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mathias Chikawe akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (hayupo pichani) kufungua mkutano wa siku mbili wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Bella Bird akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Mfumo wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika utakavyoleta maendeleo katika nchi za Afrika leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akitoa neno la shukrani mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Mfumo wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika leo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Bella Bird (kushoto) mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Mfumo wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika leo jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi na Mkurgenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bongo Live masuala ya ujumbe mfupi wa simu na mifumo ya simu Taha Jiwaji (kushoto) akifafanua kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) namna kampuni yake inavyofanya kazi mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Mfumo wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika leo jijini Dar es Salaam.
Angelina Misso (katikati) akifafanua jambo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) namna Chuo Kikuu cha Dar es salaam Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (CoICT) kinavyofanya kazi na sekta mbalimbali katika matumizi sahihi ya takwimu huria mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili unaohusu Mfumo wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Biasha Mkenga kutoka Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (CoICT), Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa (wa kwanza mstari wa mbele kushoto) akifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mkutano wa siku mbili wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika unaofanyika nchini katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi wa Makatibu Wakuu na Manibu Katibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali wakifuatilia wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mkutano wa siku mbili wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika unaofanyika nchini katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) akiongea na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Mfumo wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akiongea na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Mfumo wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika leo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati mstari wa mbele walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Mfumo wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika leo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati mstari wa mbele walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya mkutano huo mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Mfumo wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

 NA BEATRICE LYIMO- MAELEZO
4/9/2015
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete amawaasa Asasi za kiraia na Taasisi binafsi kuwa wazi katika masuala yao katika shughulizao kwa wananchi ili kuleta maendeleo nchini.
Rais Kiwete amesema hayo wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Rais Kiwete amesema kuwa mkutano wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika ni wa kwanza na wa aina yake  kufanyika Barani Afrika na Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji ambapo imeshirikiana na Benki ya Dunia katika kuandaa mkutano huo.
Dkt. Kikwete ameongeza kuwa heshima hiyo imetokana na Tanzania kujiunga na Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi (OGP) unaolenga kuifanya Serikali kuwa wazi na hivyo kuleta uadilifu na uwajibikaji katika kuwahudumia Wananchi. 
“Katika utekelezaji wa Mpango wa OGP, Tanzania iliweka kipaumbele katika kuanzisha Tovuti ya Takwimu Huria itakayoweka wazi takwimu mbalimbali za Serikali na Taasisi zake” amefafanua Rais Kikwete.
Naye Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Bella Bird amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kujadiliana kuhusu mfumo wa Takwimu Huria na jinsi utakavyoleta maendeleo hususani kwa nchi za Afrika ikiwemo mwenyeji Tanzania. 
Kwa upande wake Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema kuwa Takwimu huria itawasaidia wananchi kujua nini kinaendelea katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya maji, elimu na afya ambazo ndio sekta zinazogusa jamii kwa ukaribu na kupelekea kuanza na sekta hizo.
Pia ameongeza kuwa sera ya Takwimu huria ipo kwenye matayarisho na inategemewa kuanza kutumika baada ya miezi sita ijayo na hivyo kumfanya mwanachi kuweza kuingia kwenye mtandao na kujua matatizo yanayoikabili jamii.
Halikadhalika Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wea mkutano huo amesisitiza kuwa nchi za Afrika zitumie takwimu huria kwa ajili ya kuleta maendeleo katika nchi zao kwani zinasaidia kupata fursa mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa ajira na pia kumfanya mwananchi kufanya uchambuzi wa kutosha kwa kufuata viwango na kujua hali halisi juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea katika nchi taifa yao.
Mkutano huo unaoendelea jijini Dar es salaam unajumuisha takribani nchi 30 kutoka ndani na nje ya Afrika kwa kushirikisha wawakilishi mbalimbali kuwakilisha Serikali zao,  Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi, Taasisi za Elimu ya Juu pamoja na Washirika mbalimbali wa Maendeleo.







No comments:

Post a Comment