Pages

Pages

Pages

Sunday 6 September 2015

NINI CHA KUJIFUNZA TOKA MAJIRANI ZETU NA FAIDA YA KUKUTANA KUTANGAZA NCHI NI IPI?

1-Maonesho ya uzuri ya Wakenya- pic by F Macha 2015 
  Fahari ya Kenya. Maonesho ya uzuri na urembo 

Habari na picha za Freddy Macha

Tamasha la “Kenya in the Park”- Jumamosi iliyopita, tarehe 29 Agosti 2015, lilifana sana. Tamasha kama hili limewahi pia kufanywa mara nyingi na Ghana. Faida yake nini? 
1. Kutangaza nchi. Kuendeleza wajasiriamali, elimu, wasanii, nk 

2. Kukutanisha wananchi. Kuwaunganisha. Urafiki. Uzalendo. Kujuana. NETWORKING, kwa Kimombo. 
3. Wageni huwajua na kutaka kuwatembelea. Utalii, kuwekeza na kuunga mkono miradi mbalimbali. Tamasha hili lilikuwa na watu wa nchi mbalimbali waliokiri kuifagilia sana Kenya! Ulikuwa pia wakati Kenya ilipoongoza kwa medali za Riadha, mjini Beijing. 
4. Sanaa na Michezo. Vigezo vinavyokuuza uchumi. Tutafakari namna mataifa kama Jamaica na Brazil yanavyofahamika kutokana na fani hizi
5. Kurahisisha mawasiliano ili panapotokea janga au zuri iwe rahisi kueleweshana. Starehe, vifo, kampeni za Ebola, Malaria, UKIMWI nk 
6. Paki zina urahisi zaidi kuliko maholi ya kifahari yenye gharama kubwa. Yote yanayofanyika katika kumbi za densi yanawezekana viwanja safi vya Uingereza : densi, vyakula, vinywaji, kujamiiana, nk. 
3-Mkenya na mkewe wakifurahia ubwabwa - pic by F Macha 
Mkenya na mkewe wakifurahia siku hiyo uwanja wa West Ham, London. 2-Mohammed Juma wa Mombasa na Nyama Choma- pic by F Macha 
Mohammed Juma wa Mombasa akishughulika na nyama choma, ndizi mzuzu za kuoka nk. 5-Lydia Olet akiwa na Wacheza sarakasi wa Ghana- pic by F Macha 2015 
Mtayarishaji wa maonesho, msanii na mwanahabari, Lydia Olet, akiwa na wacheza sarakasi toka Ghana 
Baadhi ya mambo yaliyofanywa na Wakenya yalikuwa 
1. Michezo kama ngumi 
2. Starehe za watoto 
3. Warsha za Ngoma asilia za Kiafrika na Kenya 
4. Wasanii toka nchi nyingine za Afrika 
5. Maelezo ya Wakenya wanaofanya ya maana Uingereza, nini kiini cha Wimbo wao wa Taifa, nk 
6. Hotuba fupi ya Balozi Mhe. Lazarus Amayo 
7. Biashara za mali asilia toka Kenya kama kanga, vitenge, fulana nk 
8. Maonesho ya uzuri, mavazi, sanaa na urembo 
9. Maonesho ya muziki. Wanamuziki toka Kenya, Uingereza, Congo, Uganda, Tanzania, Sierra Leone, Ghana, nk 
10. Usingaji na masuala ya Afya 
11. Vyakula mbalimbali vya Kenya : Ugali, Nyama Choma, Sukumawiki, Chapati, Makongoro, Ubwabwa nk 
12. Vyakula vya nchi nyingine Afrika Mashariki mathalan, Ethiopia.
  10-Fulana ya Kiswahili - pic by F Macha 2015 12-Mkenya akifurahia siku kwa kinywaji- pic by F Macha 2015
Mkenya akichangamkia hali kwa kinywaji 7-Deo Kamugisha akiwa na Mganda na Mtanzania Abdallah- pic by F Macha
Wana Afrika Mashariki. Mwanahabari mkongwe , Deo Kamugisha (wa kwanza kulia) akiwa na Mtanzania Abdallah (kwanza kushoto) na rafiki toka Uganda 6-Lydia Makale and Septimus Prime - pic by F Macha 2015
Mkenya Lydia Makale akiwa na mwanarapu chipukizi wa London, Septimus Prime 4-Wapambe wa Kenya na mwandishi F Macha
Mwana Kitoto na Wapambe husika wa tukio... Bango la Kenya in the Park- Aug 2015 8-Wasanii nyuma ya jukwaa- pic by F Macha 2015
Baadhi ya wasanii nyuma ya jukwaa kabla ya kufanya maonesho yao 9-Muhindi na fulana ya Kenyan Airways- pic by F Macha 11-Bibi wa KiKenya akifurahia msosi- pic by F Macha
Mamii wa Kenya akifurahia msosi. Ubwabwa. 13- Mwanamuziki Billy Mwangura toka Mombasa- pic by F Macha 2015
Mzawa wa Mombasa, Billy Mwangura, mpiga besi wa bendi la Afrika Jambo 14-Mpiga gitaa Kawele katikati na Waganda- pic by F Macha 2015 
Mpiga gitaa mashuhuri na kiongozi wa bendi ya Afrika Jambo, Kawele Mutimanwa akiwa na wapambe toka Uganda. Ghana in the Park-2014
Waghana wakisheherekea siku yao (kama hii) mwaka jana. Picha ihsani ya Akwaaba UK. http://akwaabauk.com/wp-content/uploads/2014/08/IMG_0469.jpg F Macha na Steve Kasamba wa Uganda - pic by JJ Adamson 2015
Mwana Kitoto na msanii wa ACD Arts, Steven Kasamba toka Uganda. Picha na J J Adamson wa Africans in London TV. 

  Habari zaidi tembelea: www.kenyainthepark.com

No comments:

Post a Comment