Pages

Pages

Pages

Tuesday 29 September 2015

MATAIFA YASHUKU IDADI YA WALIOFARIKI MECCA

Mahujaji
Iran ni moja ya nchi zilizokosoa sana Saudi Arabia kutokana na mkasa huo
Maafisa katika mataifa kadha wamesema zaidi ya watu 1,000 walifariki kwenye mkanyagano karibu na Mecca wakati wa kuhiji.

Idadi hiyo inazidi ile iliyotolewa na maafisa wa Saudia ambayo ni 769.
Afisa mmoja nchini Nigeria ameambia BBC kuwa miili Zaidi ya 1,000 imeondolewa kutoka eneo la maafa na kupelekwa kwenye mochari zilizoko jiji la Jeddah.
Maafisa nchini Indian, Pakistan na Indonesia pia wamenukuliwa wakisema wanaamini idadi ya waliofariki ni zaidi ya 1,000.
Afisa wa haji nchini Nigeria kutoka Kano, Abba Yakubu, ameambia mwandishi wa BBC Yusuf Ibrahim Yakasai kwamba amekuwa Jeddah, ambako miili ya waliofariki kwenye mkasa huo wa Alhamisi ilipelekwa.
BwYakubu amesema kwa jumla, lori 14 zilizokuwa zimejaa miili zilifika mjini humo.
Aliongeza kuwa kufikia sasa miili 1,075 imetolewa kutoka kwenye lori 10 na kupelekwa kwenye fuo mbalimbali. Lori nne bado hazijashughulikiwa.
Mataifa kadha yamekosoa jinsi maafisa nchini Saudia walishughulikia mkasa huo, hasa mshindani mkuu wa Saudi Arabia eneo la Mashariki ya Kati Iran, ambayo ilipoteza watu 228.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa India Sushma Swaraj ameandika kwenye Twitter kwamba maafisa wa Saudia wamechapisha picha 1,090 za mahujaji waliofariki.
Mahujaji
Image captionMkanyagano ulitokea katika eneo la Mina ambako kuna nguzo za Jamarat
Maafisa wa Pakistan na Indonesia pia wamedai kupokea zaidi ya picha 1,000.
Maafisa wa Saudia bado hawajafafanua tofauti iliyopo kati ya takwimu hizo.
Mkanyagano huo ndio mbaya zaidi kutokea wakati wa haji katika kipindi cha miaka 25.
Kufikia Alhamisi, hii ndiyo idadi ya watu waliofariki kutoka barani Afrika na uraia wao kwa mujibu wa shirika la AFP.
Morocco: 87
Misri: 55
Nigeria: 54
Cameroon: 20
Niger: 22
Ivory Coast: 14
Chad: 11
Somalia: 8
Algeria: 8
Senegal: 5
Libya: 4
Tanzania: 4
Kenya: 3
Burkina Faso: 1
Burundi: 1
Tunisia: 1
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment