Pages

Pages

Pages

Thursday 3 September 2015

BESIGYE KUPEPERUSHA BENDERA YA FDC


Kiongozi wa zamani wa FDC, Kiiza Besigye
Rais wa zamani wa Chama cha upinzani nchini Uganda, Forum for Democratic Change, FDC, Dokta Kizza Besigye ameibuka mshindi katika kinyang'anyiro cha kupeperusha bendera dhidi ya Rais wa sasa Meja Jenerali, Mugisha Muntu.
Besigye amejizoela kura 718 dhidi ya 289 katika uchaguzi uliokuwa vuta nikuvute uliofanyika jijini Kampala
Wajumbe wa FDC walikutana jumatano jijini Kampala kumchagua mgombea atakayewakilisha chama hicho katika uchaguzi mkuu mwakani.Rais wa sasa wa FDC Meja Jenerali Mugisha Muntu alipambana na Rais wa zamani wa
Chama hicho Kizza Besigye katika kinyang'anyiro hicho.
Dokta Besigye amejitosa tena kwenye mchakato wa Urais utakaofanyika mwakani.
Besigye sasa ataomba ridhaa ya wanachama kutoka muungano wa Vyama vya upinzani,TDA.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment