Pages

Pages

Pages

Monday 24 August 2015

WALIOTIBUA SHAMBULIZI UFARANSA WATUNUKIWA

Medali kwa waliotibua shambulizi Ufaransa
Rais wa Ufaransa Francois Hollande amatoa tuzo la juu zaidi nchini Ufaransa kwa Waamerika wanne ambao walitibua shambulizi la kigaidi kwenye treni ya mwendo wa kasi kwenda mjini Paris siku ya Jumamosi.

Mwanajeshi Mmarekani ambaye alijeruhiwa Spencer Stone alipomuangusha mwanamgambo huyo sakafuni , alipewa tuzo hilo pamoja na Waamerika wengine na Muingereza mmoja ambao wote wametajwa kuwa mashuja.

Mshukiwa wa ugaidi

Bwana Hollande alisema kuwa kungetokea maafa kwenye treni hiyo iwapo abiria hao hawangechukua hatua.
Waziri mkuu wa Ubelgiji Charles Michel na balozi wa Marekani nchini Ufaransa Jane Hartley walishudhuia sherehe hizo.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment