Pages

Pages

Pages

Saturday 22 August 2015

MUSEVENI AMSUTA RAILA ODINGA KUHUSU SUKARI

Rais Yoweri Museveni wa Uganda
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemsuta kiongozi wa upinzani wa Kenya, Raila Odinga, kwa kupinga mkataba wa uuzaji wa sukari uliotiwa sahihi majuzi.
Museveni alisema kuwa Odinga hafaaamu anachokisema.
'Hhata ndugu yangu odinga anazungumzia maswala ya sukari,bila kufahamu ukweli wa maswala hayo,'' Museveni.
Kenya imekuwa ikizuia sukari yetu na mahindi ilihali Uganda imekuwa ikiagiza bidhaa za thamani kubwa pasi na kujali kuwa inawasaidia kujiendeleza.
''Wewe ni mkurugenzi wa kampuni ilihali kazi yako kubwa ni kuzuia sukari ya Uganda isiingie Kenya.

Kenya inanakisi ya takriban tani 250,000 za sukari kukidhi mahitaji ya raia wake.

Hii ni akiligani jamani ?''aliuliza Museveni.
'Nafikiri nitampigia Raila simu nimwambie kuwa sukari ya Uganda itaingia Kenya sawa na vile mali ya Kenya inaingia Uganda bila vizingiti' aliongezea Museveni.
Rais Museveni aliyasema hayo alipokuwa akihutubia wageni waalikwa na wabunge wa bunge la Afrika Mashariki lililoanza vikao vyake jiji Kampala Uganda.
Museveni alisema mataifa wanachama wa muungano wa kanda hii ya Afrika Mashariki na kati sharti yafuate kanuni za muungano ikiwemo Kenya.

Museveni amusuta Raila kuhusu Sukari ya Uganda

''Kenya inasafirisha mali ya thamani ya dola milioni 700 kuingia Uganda na kununua bidhaa zenye thamani ya dola milioni 150 kutoka Uganda, Ninamshukuru rais Kenyatta kwa kuondoa mashrti makali na vizuizi vilivyokuwa vinakataza bidhaa za Uganda Kuingia Kenya.alisema Museveni.
Uganda kwa sasa inasaga sukari tani 450,000 huku ikitumia takriban tani 320,000 na hivyo inasalia takriban tani 145,000 za sukari.
Hii ndiyo sukari ambayo sasa itaruhusiwa kuuzwa nchini Kenya.
Kwa Upande wake Kenya inazalisha takriban tani 600,000 ya sukari huku ikihitaji kati ya tani 800,000 na 850,000 kwa hivyo inanakisi ya takriban tani 250,000 za sukari kukidhi mahitaji ya raia wake.

Uganda kwa sasa inasaga sukari tani 450,000 huku ikitumia takriban tani 320,000 na hivyo inasalia takriban tani 145,000 za sukari.

Bwana Odinga amekuwa akidai kuwa sukari iliyokubalika kuingia Kenya kutoka Uganda sio sukari inayoundwa nchini humo bali ni sukari inayotokea Brazil na kupakiwa katika magunia ya sukari ya makampuni ya kusaga sukari ya uganda kwa minajili ya kukwepa kulipa kodi.
Wazo hilo limepuziliwa mbali na serikali ya Kenya ambayo imekuwa ikisisitiza kuwa sukari ya Uganda itaendelea kuingia Kenya chini ya mpango wa jumuia ya Afrika Mashariki COMESA.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment