Pages

Pages

Pages

Sunday 2 August 2015

MGOGORO WA UONGOZI WALIKUMBA KUNDI LA TALEBAN

Wapiganaji wa Taleban

Msemaji wa baraza kuu la kundi la Taliban nchini Afghanistan ameimbia BBC kuwa hawakuombwa ushauri wakati wa uteuzi wa hivi majuzi wa kiongozi mpya kufuatia kifo cha mwanzilishi wake Mullar Omar.
Msemaji wake Mullah Abdul Manan Niazi anasema kuwa baraza hilo litafanya mkutano ili kumchagua kiongozi mpya.
Wapiganaji wa Taleban kutoka Afghanistan
Siku ya Alhamisi taarifa za Taliban zilisema kuwa Mullah Akhtar Mansour alikuwa amechaguliwa kuliongoza kundi hilo.
Baadhi ya wanachama wa Taliban wamewalaumu wanachama wengine nchini Pakistan kwa kuwalazimishia Mullah Mansour kama kiongozi wao.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment