Pages

Pages

Pages

Saturday 22 August 2015

KOREA KASKAZINI SASA YAITISHIA KOREA KUSINI


Huku msukosuko ukiendelea kushuhudiwa katika rasi ya Korea, Korea Kusini inasema kuwa Korea Kaskazini imepeleka silaha kwenda kwa mpaka baada ya kutoa vitisho vya kuharibu vipasa sauti vinavyotangaza propaganda kutoka Korea Kusini.
Muda wa mwisho uliotangazwa na Korea Kaskazini wa kutaka kuondolewa kwa vipasa sauti hivyo unatarawajiwa kukamilika saa chache zinazokuja.



Vipasa sauti vya Korea Kusini

Korea Kusini inasema kuwa itajibu vikali . Ndege zake za kivita zimekuwa zikiruka pamoja na za Marekani karibu na mpaka.
Mwandishi wa BBC nchini Korea Kusini anasema kuwa ni muda uliotangazwa na korea kaskazini ndio unaoifanya hali kuwa hatari zaidi.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment