Pages

Pages

Pages

Sunday 2 August 2015

KAMPUNI YA MAFUTA SOMALIA YACHUNGUZWA


Idara ya Uingereza inayopeleleza udanganyifu mkubwa, inachunguza tuhuma za rushwa, kuhusu kampuni ya mafuta ya Uingereza inayofanya kazi Somalia.
Mwenyekiti wa kampuni hiyo,Soma Oil and Gas,Michael Howard,ni kiongozi wa zamani wa chama tawala cha Conservative.
Soma Oil and Gas inasema, siku zote imefanya shughuli zake kwa njia halali, na inashirikiana kikamilifu na uchunguzi huo.
Kwenye tovuti yake, idara ya upelelezi imetoa wito kwa wale wanaojua siri ya kampuni hiyo, kuwasiliana nayo.
Mwaka jana wachunguzi wa Umoja wa Mataifa, walisema wana wasiwasi, kuwa kandarasi iliyotiwa saini na Soma Oil and Gas, haikutolewa hadharani.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment