Pages

Pages

Pages

Friday 21 August 2015

KAMATI YA UCHAGUZI DRFA YAPANGUA AGIZO LA KAMATI YA UCHAGUZI TFF KUSIMAMISHA UCHAGUZI WA TEFA.

Kamati ya uchaguzi ya chama cha soka mkoa wa Dar e salaam DRFA,imeshindwa kutekeleza agizo la lililotolewa na mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF la kusimamisha mchakato wa uchaguzi wa chama cha soka wilaya ya temeke TEFA uliopangwa kufanyika jumapili agosti 23/2015.

Baada ya kupitia kwa umakini kanuni za uchaguzi za TFF za mwaka 2013 ibara ya 6, na kujiridhisha kuwa hakuna kipengele chochote kinachoruhusu kamati ya uchaguzi ya TFF kuingilia kati mchakato wa uchaguzi wa TEFA,Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya DRFA,Rashid Saadallah,(mwanasheria ),amemuandikia barua mwenyekiti wa uchaguzi wa TFF,Aloyce Komba kumjulisha hilo na kumueleza kuwa mchakato huo sasa utaendelea kama ulivyopangwa kufanyika jumapili agosti 23/2015.
Mwenyekiti huyo wa uchaguzi DRFA,amesema mpaka sasa taratibu na maandalizi yote kuelekea uchaguzi huo wa jumapili yamekamilika ikiwemo usikilizwaji wa rufaa mbalimbali na kuzitolea uamuzi,hivyo  kitendo cha kuingilia kati mchakato huo ni kinyume cha utaratibu,kwa kuwa TEFA ni mwanachama wa DRFA na siyo wa TFF.

No comments:

Post a Comment