Pages

Pages

Pages

Sunday 23 August 2015

IRAN NA UINGEREZA KUFUNGUA BALOZI ZAO


Uingereza na Iran zinatarajiwa kufungua balozi kwenye miji yao mikuu licha ya kuwepo uhusiano mbaya katika ya Iran na nchi za magharibi.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Iran Philip Hammond anatarajiwa kuwasili mjini Tehran kwa sherehe hizo.
Atakuwa afisa wa kwanza wa ngazi ya juu zaidi wa Uingereza kuzuru Iran tangu miaka 12 iliyopita.

Ubalozi wa Uingereza ulivamiwa mwaka 2011

Ubalozi wa uingereza ulifungwa mwaka 2011 wakati ulisakwa na waandamanaji.
Makubaliano ya nyukia ya mwezi uliopita kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani yametoa njia ya kuboreshwa kwa uhusiano kati yao.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment