Pages

Pages

Pages

Friday 28 August 2015

ARSENAL USO KWA USO NA BAYERN MUNICH UEFA CHAMPIONS LEAGUE

Arsenal na Bayern Munich zilipokutana msimu uliopita
Baada ya jana kufanyika droo ya makundi ya klabu bingwa barani Ulaya, mashabiki wa soka watapata fursa ya kushuhudia baadhi ya historia zikijirudia huku zingine mpya zikiandikwa.
Arsenal kwa mara ya tatu katika misimu minne, itavaana na Bayern Munich baada ya kupangwa kundi moja.
Wakati hayo yakijiri, mchezaji mpya wa Manchester Utd Memphis Depay atapata fursa ya kupambana na timu yake ya awali ya PSV Eindhoven ya uholanzi baada ya timu hizo kupangwa kundi moja.
Na ligi kuu ya Hispania La liga, pia mwaka huu imeweka historia baada ya mwaka huu kuingiza timu tano katika hatua hiyo ya makundi, jambo ambalo halikuwahi kutokea hapo awali.
Timu hizo ni Real Madrid, Barcelona, Atletico Madrid, Valencia pamoja na Sevilla.
BBC

No comments:

Post a Comment