Pages

Pages

Pages

Tuesday 28 July 2015

RAIS WA FFB KUWASILI LEO


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Burundi (FFB), Reverien Ndikuriyo anatarajiwa kuwasili leo saa 5 usiku jijini Dar es salaam kwa shirika la Ndege la Rwanda Air.
 
Ndikuriyo anatarjaiwa kuwa na mazungumzo na Rais wa TFF, Jamali Malinzi kisha atashuhudia michuano ya kombe la Kagame inayoendelea kutimua vumbi jijini Dar es salaam ikiwa katika hatua ya robo fainali kwa sasa.

Aidha Vicent Nzamwita Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Rwanda (FERWAFA) anatarajiwa kuwasili nchini alhamis akiambatana na kocha wa timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi) John McKinstry.

Rais wa FERWAFA anatarajiwa kuwa na mazungumzo na Rais wa TFF, Jamal Malinzi na baadae kuhudhuria michuano ya Kombe la Kagame inayoendelea nchini Tanzania.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

No comments:

Post a Comment