Pages

Pages

Pages

Friday 31 July 2015

NIGERIA YATEUA JENERALI MPYA WA JESHI

Jeneral Iliyasu Isah Abbah
Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria

Nigeria imemteua Jenerali mpya kuongoza kikosi cha kimataifa kilichoundwa kwa ajili ya kupamba na kundi la wanamgambo wa Boko Haram.

Meja Jeneral Iliyasu Isah Abbah ataongoza kikosi hicho kitakachokuwa na askari takriban 9000 kutoka nchi tano.
Nigeria imemchagua General huyo mpya kwa lengo la kupambana na wanamgambo hao wa kundi la kigaidi la Boko Haram.
Kikosi hicho kinatarajiwa kuwa na ofisi zake katika mji mkuu wa Chad N'Djamena na wanatarajiwa kuendesha operesheni zake kikamilifu kuanzia mwezi ujao.
Nigeria na majirani zake wamekuwa wanajitahidi kupambana na wapiganaji wa Boko Haram ambao wameua watu wapatao elfu ishirini.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment