Pages

Pages

Pages

Friday 24 July 2015

LUKUVI ATANGAZA KUFUTA HATI ZA ARDHI

Waziri wa Ardhi, William Lukuvi
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema atafuta umiliki kwa maeneo  nchini ambayo yametekelezwa kwa zaidi ya miaka 10 bila ya kuendelezwa.

Lukuvi alitangaza mpango huo katika Kijiji cha Tungamalenga kilichopo Wilaya ya  Iringa mkoani hapa, alikokwenda kusikiliza mgogoro wa ardhi baina ya wananchi, wawekezaji , wafugaji na wakulima.
Alisema ametoa agizo hilo nchi nzima kwa watu  walionunua ardhi za vijiji zaidi ya hekari 50 na kushindwa kuziendeleza hivyo kugeuka mapori.
Alisema amewaagiza maofisa wa ardhi wa halmashauri na wizara yake kufuatilia ili kujua watu hao wamenunua ardhi hiyo kwa malengo yapi,  lini na wameendeleza kwa kiasi gani hadi sasa.
Lukuvi ambaye pia ni Mbunge wa Ismani anayemaliza muda wake, alisema kabla ya kufuta umiliki wa maeneo hayo, maofisa hao watatakiwa kuwapa notisi wamiliki waliyoshindwa kuyaendeleza.
“Kazi ya kuweka akiba ya ardhi haiwezi kuwa kazi yenu ninyi lakini haiwezekani ukatoka jijini Dar es Salaam ukanunua ekari 100 Tungamalenga ukasema unajiwekea akiba ya miaka 20 ijayo mimi sitakubali, " alisema na kusisitiza kuwa:
"Serikali ya kijiji lazima iwe na akiba ya ardhi kwa vizazi vijavyo na sisi kama serikali kuu lazima tuwe na akiba ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa kitaifa. 
Akijibu malalamiko ya wakazi wa kijiji hicho, Lukuvi    aliwaagiza maofisa Ardhi wa Halmashauri ya wilaya hiyo kwenda kutoa ufafanuzi wa eneo ambalo limepangwa na serikali kuu na lililoachwa kama akiba ya kijiji.
Kwa upande mwingine aliwaonya viongozi wa vijiji wasiuze ardhi yote kwa wawekezaji ili kudonoa migogoro kwenye maeneo yao.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment