Pages

Pages

Pages

Thursday 23 July 2015

KOMBE LA KAGAME: YANGA, GOR MAHIA ZAGOMEA MICHEZO

Amisi Tambwe wa Yanga akifanyiwa madhambi na mchezaji wa Gor Mahia katika mechi ya ufunguzi Julai 18, 2015.

Na Daniel Mbega wa www.brotherdanny.com

YANGA, Gor Mahia ya Kenya, Limbe Leaf Wanderers ya Malawi na Al Hilal ya Sudan ndizo timu pekee ambazo zina historia ya kususia mechi wakati mashindano ya Kombe la Kagame yakiwa yanaendelea.

Kwa nyakati tofauti, timu zimepata kususia mechi zao kwa sababu mbalimbali, ingawa ni Yanga pekee ambayo ilipata kuadhibiwa vikali kwa kufungiwa kushiriki kwa miaka mitatu mwaka 2008.
Yanga ilikuwa imesusia mechi yake ya kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya Simba mwaka 2008, lakini Limbe Leaf ilisusia mwaka 1981, Gor Mahia iligomea mchezo mwaka 1982 na Al Hilal ilisusia mwaka 1994.
Ifuatayo ni kumbukumbu sahihi ya ripoti za mashindano hayo ambazo zinaonyesha namna timu hizo tatu zilivyopata kususia mechi zao:

Mwaka 1981 – Limbe Leaf yagomea penati ya Simba
Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kwa mwaka 1981 yalifanyika katika miji ya Nairobi na Kisumu nchini Kenya kati ya Januari 18 na Februari Mosi.
Jumla ya timu saba zilishiriki mashindano hayo ambazo ni Limble Leaf Wanderers (Malawi), Kabwe Warriors (Zambia) na AFC Leopards (Kenya) ambazo zilikuwa Kundi A. Kundi B lilikuwa na KMKM (Zanzibar), Simba SC (Tanzania), Nile Breweries (Uganda) na Gor Mahia (Kenya).
Mwaka 1981 Simba iliingia fainali na bao 1 na ilimaliza mashindano hayo ikiwa na bao hilo hilo moja.
Katika michuano ya awali Simba SC ilipangwa Kundi B mjini Kisumu, na iliifunga Nile Breweries ya Uganda 1-0 Januari 18, halafu ikatoka suluhu na KMKM ya Zanzibar na Gor Mahia ya Kenya.
Gor Mahia yenyewe ilianza kwa kuichapa KMKM mabao 2-0, kipigo ilichokitoa pia kwa Nile Breweries, hivyo ikakusanya pointi 5 na kuongoza kundi hilo. Simba ilishika nafasi ya pili na kufuzu kwa nusu fainali.
Kwenye nusu fainali Simba ilikutana na Limbe Leaf mjini Nairobi Januari 29, ambapo Limbe Leaf ilijipatia bao moja na wakati ikiongoza kwa goli hilo katika dakika ya 86 mlinzi wake akaunawa mpira kwenye eneo la hatari, Simba wakapata penati.
Hata hivyo, wachezaji wa timu hiyo ya Malawi walitoka nje ya uwanja kugomea penati hiyo waliyodai ilikuwa na utata. Jitihada za kuwashawishi warejee kuendelea na mechi zikagonga mwamba.
Hivyo, katika mkutano maalum Cecafa ikaamua kuipa ushindi Simba na kuipeleka katika fainali ambako ilifungwa 1-0 na Gor Mahia. Bao hilo lilifungwa na Nashon Oluoch 'Lule'.
Gor Mahia katika nusu fainali ilikuwa imeifunga Kabwe Warriors ya Zambia mabao 2-1 siku hiyo ya Januari 29.
Limbe Leaf Wanderers ilijifariji na nafasi ya mshindi wa tatu baada ya kuifunga Kabwe Warriors mabao 2-0 Januari 31.
Matokeo kamili ya mechi za mashindano hayo ni haya:

Kundi A
Limble Leaf W. 3-1 Kabwe Warriors
AFC Leopards   0-0 Limble Leaf Wanderers
Kabwe Warriors 3-1 AFC Leopards

 1.Limble Leaf Wd. 2  1  1  0  3- 1  3  [Malawi]
 2.Kabwe Warriors  2  1  0  1  4- 4  2  [Zambia]
 3.AFC Leopards    2  0  1  1  1- 3  1  [Kenya]

Kundi B
KMKM           0-2 Gor Mahia
Simba SC       1-0 Breweries
Gor Mahia      2-0 Breweries  
Simba SC       0-0 KMKM
Gor Mahia      0-0 Simba SC
Breweries      1-0 KMKM

 1.Gor Mahia       3  2  1  0  4- 0  5  [Kenya]
 2.Simba SC        3  1  2  0  1- 0  4  [Tanzania]
 3.Breweries       3  1  0  2  1- 3  2  [Uganda]
 4.KMKM            3  0  1  2  0- 3  1  [Zanzibar]

Nusu fainali
Limble Leaf W. vs Simba SC [Jan 28; Simba ilipewa ushindi wa mabao 2-0; awali ilifungwa bao 1-0 lakini Limbe Leaf Wanderers iligomea penati na hivyo Simba ikapewa ushindi]
Gor Mahia      2-1 Kabwe Warriors

Mshindi wa tatu
Limble Leaf W. 2-0 Kabwe Warriors

Fainali
Gor Mahia      1-0 Simba SC 

Mwaka 1982- Gor yapomea penati dhidi ya Leopards
Mwaka 1982 AFC Leopards ilipambana na mahasimu wao Gor Mahia kwenye nusu fainali jijini Nairobi wakati mashindano hayo yalipofanyika nchini Kenya. Hadi dakika 90 zinamalizika, matokeo yalikuwa suluhu, hivyo sheria ya penati tano tano ikabidi itumike kumpaka mshindi.
Hata hivyo, Gor Mahia iligomea sheria hiyo ikitaka uwepo muda wa nyongeza, lakini Cecafa ikashikilia kwamba lazima matuta yatumike. Gor ikagoma, ikabidi AFC Leopards ipewe ushindi wa mezani wamabao 2-0 na kusonga fainali ambako ilitawazwa kuwa mabingwa baada ya kuichapa Rio Tinto ya Zimbabwe bao 1-0.
Mashindano ya mwaka 1982, ambayo yalifanyika kuanzia Februari 13 hadi 25, yalishirikisha timu nane zilizogawanywa katika makundi mawili ambapo Kundi A lilikuwa mjini Nairobi likihusisha timu za AFC Leopards, Rio Tinto ya Zimbabwe, Ujamaa ya Zanzibar na Information Club ya Somalia.
Kundi B lilikuwa mjini Kisumu likihusisha timu za Gor Mahia, Bata Bullets, Yanga na Kampala City Council.
Matokeo kamili ya mashindano hayo ni kama ifuatavyo:

Kundi A [Nairobi]
13- 2 AFC Leopards   2-0 Rio Tinto
14- 2 Ujamaa         1-0 Information Club
16- 2 Rio Tinto      4-1 Ujamaa     
17- 2 AFC Leopards   2-0 Information Club
19- 2 Ujamaa         0-3 AFC Leopards  
20- 2 Rio Tinto      1-1 Information Club

 1.AFC Leopards    3  3  0  0  7- 0  6  [Kenya]
 2.Rio Tinto       3  1  1  1  5- 4  3  [Zimbabwe]
 3.Ujamaa          3  1  0  2  3- 7  2  [Zanzibar]
 4.Information C.  3  0  1  2  1- 4  1  [Somalia]

Kundi B [Kisumu]
13- 2 Gor Mahia      1-1 Bata Bullets
14- 2 Young Africans 2-1 Kampala City Council
16- 2 Gor Mahia      1-0 Kampala City Council
17- 2 Young Africans 1-0 Bata Bullets
19- 2 Gor Mahia      3-1 Young Africans         
20- 2 Bata Bullets   2-0 Kampala City Council

 1.Gor Mahia       3  2  1  0  5- 2  5  [Kenya]
 2.Young Africans  3  2  0  1  4- 4  4  [Tanzania]
 3.Bata Bullets    3  1  1  1  3- 2  3  [Malawi]
 4.Kampala CC      3  0  0  3  1- 5  0  [Uganda]

Nusu fainali
22- 2 AFC Leopards   2-0 Gor Mahia   
23- 2 Rio Tinto      2-1 Young Africans

Mshindi wa tatu
25- 2 Gor Mahia      2-1 Young Africans

Fainali
25- 2 AFC Leopards   1-0 Rio Tinto

Mwaka 1994 – Al Hilal yagoma kucheza na Merreikh
NIMEWAHI kuandika huko nyuma kwamba hakuna michuano ya KLabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati iliyokuwa na mizengwe na upendeleo wa wazi kama ya mwaka 1994. CECAFA ilifumbia macho mambo maovu kabisa kwenye kandanda, ikiwabeba wenyeji kwa mbeleko ya chuma hadi kufanikisha azma yao.
Kwanza kabisa Silver Strikers ya Lilongwe, Malawi iliwasili siku chache kabla ya mashindano lakini ilikataliwa na Katibu Mkuu wa CECAFA James Tirop wa Kenya kwa maelezo kwamba ilichelewa kujiandikisha;
Gor Mahia ya Kenya ilichelewa kuwasili katika mechi ya ufunguzi dhidi ya El Merreikh, lakini haikuadhibiwa;
Kwa hiyo Silver Strikers ilibakia mjini Khartoum kwa siku chache kwa matumaini ya kuruhusiwa kushiriki bila mafanikio, hatimaye ikarejea kwao ikiwa imepoteza gharama nyingi.
Kutokana na hali hiyo ya ubabashaji, Malawi ilijitoa CECAFA, ikifuatia hatua ya awali ya Zambia na Zimbabwe, na hazikurejea tena, badala yake zikajiunga na Shirikisho la Soka Kusini mwa Afrika (COSAFA).
Michuano ya mwaka 1994 ilifanyika katika miji ya Khartoum na Port Sudan. Kundi A lililokuwa mjini Khartoum lilizishirikisha timu za El-Merreikh (Sudan), Simba (Tanzania), Express (Uganda) na Gor Mahia (Kenya).
Kundi B la mjini Port Sudan lilikuwa na mabingwa watetezi, Yanga (Tanzania), El-Hilal Port Sudan, Electric (Ethiopia) na Shangani (Zanzibar).
Michuano hiyo iliyoanza Januari 8 na kumalizika Januari 20 iliingia dosari Januari 14 wakati Simba, ikiwa inaongoza kwa mabao 2-1 dhidi ya El-Merreikh, ilizimiwa taa uwanjani na wachezaji wake kupigwa na mashabiki, ambapo kiungo Nico Kiondo alichomwa kisu.
Simba, ambayo ilikuwa inaongoza katika kundi A, iliamua kujitoa mashindanoni na ilikuwa inazishauri timu nyingine za Tanzania, Yanga na Shangani zijitoe. Hata hivyo, timu hizo mbili hazikujitoa.
Kwa hali hiyo, El-Merreikh iliyokuwa inashika nafasi ya pili kwenye kundi hilo, sasa ilipangiwa kucheza na mshindi wa pili wa kundi B, El-Hilal. Lakini katika hatua ya kushangaza, El-Hilal iligoma kucheza na El-Merreikh kwa madai kwamba hiyo haikuwa timu ambayo ilipaswa kupambana nayo na hivyo Shangani iliyoshika nafasi ya tatu kwenye kundi B ikapambana na El-Merreikh katika nusu fainali, ambapo ilifungwa bao 1-0.
Yanga nayo ilibidi ipambane na Express waliokuwa washindi wa tatu kwenye kundi A. Katika mchezo wa nusu fainali, Yanga ilitolewa na timu hiyo ya Uganda kwa penati 5-4 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 hadi muda wa ziada, hivyo ikawa imeutema ubingwa huo iliouchukua nchini Uganda mwaka 1993. Katika kutafuta mshindi wa tatu, Yanga iliifunga Shangani mabao 2-1.
El-Merreikh ndiyo iliyotwaa ubingwa huo kwa kuifunga Express mabao 2-1 kwenye fainali.
Kwa kweli michuano hiyo ilikuwa na dosari kubwa, kwani tangu awali ilionekana wazi kwamba Wasudani walikuwa wanapendelewa na wala CECAFA haikuweza kuchukua hatua zozote za tahadhari hata pale wachezaji wa Simba walipofanyiwa fujo.
Hebu tuangalie namna mashindano hayo yalivyokwenda:
08/01/1994:- Shangani 0 vs El-Hila 1
09/01/1994:- Yanga 0 vs Electric 0
09/01/1994:- Simba 1 vs Express 2
09/01/1994:- El-Merreikh 1 vs Gor Mahia 1
11/01/1994:- Shangani 2 vs Electric 1
11/01/1994:- Express 1 vs El-Merreikh 2
12/01/1994:- Yanga 1 vs El-Hilal 1 (Fumo Felician/Amir Moussa)
12/01/1994:- Simba 1 vs Gor Mahia 0
14/01/1994:- *Simba 2 vs El-Merreikh 1 (Ramadhani Lenny, Nteze John/?) - mchezo ulivunjika dakika ya 88).
14/01/1994:- Yanga 2 vs Shangani 1
14/01/1994:- Express 1 vs Gor Mahia 0
14/01/1994:- El-Hilal 0 vs Electric 0

Kundi A
 1.El Merreikh     3  2  1  0  3- 2  5  [Sudan]
 2.Express FC      3  2  0  1  4- 3  4  [Uganda]
 3.Simba SC        3  1  0  2  3- 2  2  [Tanzania]
 4.Gor Mahia       3  0  1  2  1- 4  1  [Kenya]
   [NB: bila mabao ambayo El Merreikh iliyopewa dhidi ya Simba]

Kundi B
 1.Young Africans  3  1  2  0  3- 1  4  [Tanzania]
 2.El Hilal        3  1  2  0  2- 1  4  [Sudan]
 3.Small Simba     3  1  0  2  2- 3  2  [Zanzibar]
 4.Mebrat Hail     3  0  2  1  0- 2  2  [Ethiopia] [aka EELPA]

NUSU FAINALI:
17/01/1994:- El-Merreikh 1 vs Shangani 0 (Zahir Abdulghani 90)
18/01/1994:- Yanga 1 (4) vs Express 1 (5) (Constantine Kimanda 14, pen: Stephen Mussa, Kenneth Mkapa, Tungaraza, Mohammed Hussein/ Robert Aloro 52, pen:)

MSHINDI WA TATU:
20/01/1994:- Yanga 2 vs Shangani 1

FAINALI:
20/01/1994:- El-Merreikh 2 vs Express 1 (Fattah Rahman Santo (mawili)/Issa Sekatawa).
[kadi nyekundu katika kipindi cha pili: Fatah El Rahman Faraq (Merreikh) na Abdul Nsubuga (Express)]


Mwaka 2008 – Yanga yagoma kucheza na Simba

KATIKA hali ya kushangaza, mwaka 2008 Yanga iligoma kupeleka timu uwanjani kucheza na mahasimu wao Simba SC katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu wa Kombe la Kagame jijini Dar es Salaam.
Hii ilikuwa mechi ya kwanza ya kimataifa kwa mojawapo ya timu hizo kuigomea pindi zikitarajia kukutana uso kwa uso, ingawa huko nyuma zilishawahi kukimbiana katika ligi na mashindano mengine ya ndani.
Kwa kawaida, timu hizi zinapokutana, mbali ya kutafuta ushindi, lakini huangalia zaidi heshima kwani kupoteza humaanisha mambo mengi, ikiwemo migogoro ya uongozi.
Sababu ambazo Yanga ilizitoa zilikuwa ni pamoja na upendeleo wa Cecafa kwa Simba na ikadaiwa kwamba kulikuwa na njama za kuhakikisha Yanga inafungwa mechi hiyo.
Mashindano ya mwaka huo yalifanyika jijini Dar es Salaam kati ya Julai 12 na 27 yakishirikisha jumla ya timu 10 zilizogawanywa kwenye makundi matatu.
Tanzania iliwakilishwa na timu mbili kwa vile ni mwenyeji, lakini Rwanda ilikuwa na wawakilishi wawili kwani APR ilikuwa inatetea ubingwa wake.
Wawakilishi wa Sudan waliondolewa, lakini timu za Société Immobilière de Djibouti – SID ya Djibouti na Denden ya Eritrea zilijitoa mapema mwezi Julai kutokana na kukabiliwa na ukata.
Kundi A lilikuwa mjini Dar es Salaam na timu za Simba, Tusker FC ya Kenya, Vital’O ya Burundi na Banaadir Telecom ya Somalia.
Kundi B lilikuwa mjini Morogoro likiwa na timu za URA ya Uganda, Rayon Sport ya Rwanda na Awassa Kenema ya Ethiopia; na Kundi C lilikuwa mjini Dar es Salaam likiwa na timu za Yanga, APR na Miembeni ya Zanzibar
Simba iliongoza Kundi A ambapo ilianza kwa kufungwa 3-2 na Tusker, Ikaiadhibu Banaadir Telecom 5-0 na kuichapa Vital’O 1-0.
Yanga nayo iliongoza Kundi C baada ya kutoka sare ya 2-2 na APR na kuifunga Miembeni 1-0, hivyo kuikwepa kiaina Simba katika robo fainali, kwani kama ingeshika nafasi ya tatu ilibidi ipambane nayo.
Katika robo fainali, Simba iliifunga APR mabao 2-0na Yanga ikaifunga Vital’O 2-0 na kutinga nusu fainali. Wengi wakabashiri kwamba huenda timu hizo zingekutana fainali.
Lakini katika nusu fainali, Julai 24 Simba ikafungwa 1-0 na URA baada ya mchezo kwenda hadi dakika 120. Bao la Eric Obua la dakika ya 111 ndilo lililoiua Simba iliyokuwa inanolewa na Jamhuri Kihwelu ‘Julio’, ambayo siku hiyo iliwakilishwa na Amani Simba, Nico Nyagawa, Ramadhan Wasoo, Kelvin Yondan, Henry Joseph, Anthony Matangalu (Emeh Izechukwu), Mohamed Banka (Ulimboka Mwakingwe), Ramadhan Chombo, Obinwa Orji (Adam Kingwande), Meshack Abel, Mussa Hassan "Mgosi". Izechukwu aliikosesha penati katika dakika ya 119.
URA iliyokuwa inafundishwa na Moses Basena, iliwakilishwa na Abbey Dhaira, Johnson Bagoole, Manco Kaweesa, Joseph Owino, David Kyobe (Martin Muwanga), Ismael Kigozi, Mussa Docca, Robert Okello (Jackson Ssenabulya), Dan Wagaluka, Henry Kiseka (Eric Obua), Samuel Mubiru.
Yanga nayo Julai 25 ikatolewa na Tusker FC kwa bao 1-0 ambalo lilifungwa na Simon Mburu kunako dakika ya 53. Siku hiyo Yanga, ambayo ilikuwa inanolewa na Mserbia Dusan Kondic, iliwakilishwa na Ivo Mapunda, Shadrack Msajigwa, Wisdom Ndhlovu, George Owino, Nurdin Bakari, Shamte Ally, Geoffrey Bonny, Athman Iddi Chugi (Vincent Barnabas), Kigi Makasi (Abdi Kassim), Boniface Ambani (Gaudence Mwaikimba), Mrisho Ngassa.
Tusker nayo, chini ya kocha Jacob ‘Ghost’ Mulee, iliwakilishwa na Boniface Otieno, Ibrahim Shikanda, John Njoroge, Joseph Shikokoti, Humphrey Okoti, Japhery Oyando (Crispin Odula), Edward Kauka, Osborne Monday, Simon Mburu, John Kio (Robson Ndondo), Justus Anene (Hassan Aden).
Sasa kulikuwa hakuna ujanja, kwani mahasimu hao walikuwa lazima wakutane kwenye mchezo wa mshindi wa tatu Julai 27. Yanga ikasema isingepeleka timu kwa vile kulikuwa na hujuma za wazi. Cecafa na wapenzi wengi wa soka wakasema hiyo ilikuwa ‘danganya toto’ kwa sababu ni kawaida kwa timu hizo kutishia hasa zinapokutana ili kuichanganya kisaikolojia timu nyingine.
Hatimaye Julai 27 ikafika, mashabiki wakajaa uwanjani wakijua lazima Yanga ingekwenda tu.
Mwamuzi Caleb Amwayi kutoka Kenya, aliyesaidiwa na Mkenya mwenzake Hesborn Mbogo na Berhe Tesfagiorgis wa Eritrea, wakasubiri hadi dakika 15 baada ya muda wa mchezo kufika, zilipopita wakapuliza kipyenga cha kumaliza mchezo na kuipa ushindi Simba.
Siku hiyo kikosi cha Simba, ambayo kwenye benchi la ufundi ilikuwa na Krasimir Bezinski wa Bulgaria, na ambacho kilipangwa kucheza na Yanga kilikuwa na Amani Simba, Kelvin Yondan, Henry Joseph, Musa Hassan, Ramadhani Chombo, Juma Jabu, Nico Nyagawa, Jabir Azizi, Emmanuel Gabriel, Antony Matangalu, na Meshack Abel.
Kutokana na hali hiyo, siku hiyo hiyo na wakati huo huo, Cecafa wakatangaza kuifungia Yanga kushiriki mashindano hayo kwa miaka mitatu na wakataka ilipe faini ya Dola 50,000!
Kwenye mchezo wa fainali, Tusker iliifunga URA mabao 2-1. Mabao ya washindi yalifungwa na ‘Ngongoti’ Joseph Shikokoti dakika ya 71 na Oscar Kadenge dakika ya 88, wakati URA ndiyo iliyokuwa imeanza kufunga katika dakika ya 23 kupitia kwa Martin Muwanga.
URA iliwakilishwa na Abbey Dhaira, Tony Mawejje, Manco Kaweesa, Joseph Owino, David Kyobe, Ismail Kogozi (Robert Okello), Dan Wagaluka, Mussa Docca (John Karangwa), Johnson Bagoole, Martin Muwanga, Samuel Mubiru.
Tusker iliwakilishwa na Boniface Otieno, Ibrahim Shikanda, John Njoroge, Joseph Shikokoti, Humphrey Okoti, Edward Kauka, Osborne Monday, Simon Mburu (Oscar Kadenge), Hassan Aden (John Kio), Crispin Odula (Kelvin Omondi), na Justus Anene.
Matokeo kamili ya mashindano hayo ni kama ifuatavyo:

Kundi A (Dar es Salaam)
12 Jul Simba 2-3 Tusker
Wafungaji: Ulimboka Mwakinwe 21, Adam Kingwande 30; Simon Mburu 9, Oscar Kadenge 45, John Keo 53.
14 Jul Vital'ô 1-2 Banaadir Telecom
Wafungaji: Kabungulu Nimubona 89; Ivan Edward 59, Nune Abdi 90.
16 Jul Tusker 1-3 Vital'ô      
Wafungaji: Kenneth Wendo 70; Eric Gatoto 16, Kabungulu Nimubona 30, Stanley Minzi 67.
17 Jul Simba 5-0 Banaadir Telecom
Wafungaji: Mussa Hassan 45+, 71, Adam Kingwande 62, Ulimboka Mwakingwe 68, Emeh Izechukwu 88.
20 Jul Tusker 5-0 Banaadir Telecom
Wafungaji: John Njoroge 14, Joseph Shikokoti 22, Jeff Oyando 74, Kenneth Wendo 76, Osborne Monday 83.
20 Jul Simba 1-0 Vital'ô
Mfungaji: Kelvin Yondan 42.

 1.Simba                 3  2  0  1  8- 3  6  (Tanzania)
 2.Tusker                3  2  0  1  9- 5  6  (Kenya)
 3.Vital'ô               3  1  0  2  4- 4  3  (Burundi)
 4.Banaadir Telecom      3  1  0  2  2-11  3  (Somalia)

Kudni B (Morogoro)
13 Jul URA 4-1 Rayon Sport 
Wafungaji: Johnson Bagole 31, 48, Robert Okello 69, Eric Obua 84; Jimmy Gatete 90.
16 Jul Awassa Kenema 1-1 URA
Wafungaji: Ftisum Tsegazab 86; Johnson Bagoole 26.
19 Jul Rayon Sport    2-0 Awassa Kenema
Wafungaji: Jean Lomani 16, Kalisa Kasse 83.

 1.URA                   2  1  1  0  5- 2  4  (Uganda)
 2.Rayon Sport           2  1  0  1  3- 4  3  (Rwanda)
 3.Awassa Kenema         2  0  1  1  1- 3  1  (Ethiopia)

Kundi C (Dar es Salaam)
13 Jul Yanga 2-2 APR
Wafungaji: Mrisho Ngasa 65, Jerry Tegete 68; Mbuyu Twite 15, 77.
15 Jul APR 1-2 Miembeni
Wafungaji: Baptiste Mugiraneza 86; Amri Kiemba 42, Maulid Ibrahim 72.
19 Jul Young Africans 1-0 Miembeni
Mfungaji: Kigi Makasi 22pen.

 1.Young Africans        2  1  1  0  3- 2  4  (Tanzania)
 2.Miembeni              2  1  0  1  2- 2  3  (Zanzibar)
 3.APR                   2  0  1  1  3- 4  1  (Rwanda)

Robo Fainali (Shamba la Bibi, Dar es Salaam)
22 Jul Simba 2-0 APR
Wafungaji: Orji Obina 80, Mussa Hassan 87.
22 Jul URA 2-0 Miembeni
Wafungaji: Ismail Kigozi 25, Sam Mubiru 71.
23 Jul Yanga 2-0 Vital'ô 
Wafungaji: Shamte Ally 14, Boniface Ambani 20.
23 Jul Tusker 0-0 Rayon Sport [7-6 pen - hakuna muda wa ziada]

Nusu Fainali (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam)
24 Jul Simba 0-1 URA [dakika 120]
Mfungaji: Eric Obua 111. Penati ya Emeh Ezechukwu ilidakwa dakika ya 119.
Simba: Amani Simba, Nico Nyagawa, Ramadhan Wasoo, Kelvin Yondan, Henry Joseph, Anthony Matangalu (Emeh Izechukwu), Mohamed Banka (Ulimboka Mwakingwe), Ramadhan Chombo, Obinwa Orji (Adam Kingwande), Meshack Abel, Mussa Hassan "Mgosi"; Kocha: Kiwelu Jamhuri.
URA: Abbey Dhaira, Johnson Bagoole, Manco Kaweesa, Joseph Owino, David Kyobe (Martin Muwanga), Ismael Kigozi, Mussa Docca, Robert Okello (Jackson Ssenabulya), Dan Wagaluka, Henry Kiseka (Eric Obua), Samuel Mubiru; Kocha: Moses Basena.
Mwamuzi: Thomas Onyango (Kenya); Mussie Kinde (Ethiopia), Hesborne Mbogo (Kenya).
25 Jul Yanga 0-1 Tusker
Mfungaji: Simon Mburu 53.
Yanga: Ivo Mapunda, Shadrack Msajigwa, Wisdom Ndhlovu, George Owino, Nurdin Bakari, Shamte Ally, Geoffrey Bonny, Athman Iddi Chugi (Vincent Barnabas), Kigi Makasi (Abdi Kassim), Boniface Ambani (Gaudence Mwaikimba), Mrisho Ngassa; Kocha: Dusan Kondic (Serbia).
Tusker: Boniface Otieno, Ibrahim Shikanda, John Njoroge, Joseph Shikokoti, Humphrey Okoti, Japhery Oyando (Crispin Odula), Edward Kauka, Osborne Monday, Simon Mburu, John Kio (Robson Ndondo), Justus Anene (Hassan Aden); coach: Jacob Mulee.
Mwamuzi: Hudu Munyemana (Rwanda); Ally Kombo (Zanzibar), Berhe Tesfagiorgis (Ethiopia).

Mshindi wa Tatu (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam)
27 Jul Simba w/o Yanga [Yanga iligoma kupeleka timu uwanjani]
Simba: Amani Simba, Kelvin Yondan, Henry Joseph, Musa Hassan, Ramadhani Chombo, Juma Jabu, Nico Nyagawa, Jabir Azizi, Emmanuel Gabriel, Antony Matangalu, Meshack Abel; Kocha: Krasimir Bezinski (Bulgaria).
Mwamuzi: Caleb Amwayi (Kenya); Hesborn Mbogo (Kenya), Berhe Tesfagiorgis (Eritrea).

Fainali (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam)
27 Jul URA 1-2 Tusker
Wafungaji: Martin Muwanga 23; Joseph Shikokoti 71, Oscar Kadenge 88.
URA: Abbey Dhaira, Tony Mawejje, Manco Kaweesa, Joseph Owino, David Kyobe, Ismail Kogozi (Robert Okello), Dan Wagaluka, Mussa Docca (John Karangwa), Johnson Bagoole, Martin Muwanga, Samuel Mubiru.
Tusker: Boniface Otieno, Ibrahim Shikanda, John Njoroge, Joseph Shikokoti, Humphrey Okoti, Edward Kauka, Osborne Monday, Simon Mburu (Oscar Kadenge), Hassan Aden (John Kio), Crispin Odula (Kelvin Omondi), na Justus Anene.
Mwamuzi: Hudu Munyemana (Rwanda); Ally Juma Kombo (Zanzibar), Hamisi Changwalu (Tanzania).

KUMBUKUMBU HIZI ZIMEANDALIWA NA MTANDAO WA www.brotherdanny.com. Tafadhali ukirejea weka chanzo cha habari.


No comments:

Post a Comment