Pages

Pages

Pages

Thursday 30 July 2015

ISRAEL YAIDHINISHA KUWALISHA WAFUNGWA KWA LAZIMA


Bunge la Israeli, limepitisha sheria ya kuwalisha kwa lazima wafungwa ambao wanashiriki mgomo na kususia kula.

Sheria hiyo ambayo ilikubalika kwa idadi kubwa kidogo ya wabunge, inawaruhusu mahakimu kuhakikisha kuwa wafungwa wanalishwa kwa lazima na pia kupata matibabu kwa lazima bila ya ruhusa ya mfungwa, mradi tu maisha yake yamo hatarini.
Wapalestina ambao wanazuiliwa katika magereza ya Israeli wamekuwa wakisusia chakula kama njia yao ya kupinga kukamatwa kwao katika miaka michache iliyopita.
Israel yaidhinisha chakula cha lazima kwa wafungwa wanaosusia chakula
Israel inahofu kuwa wafungwa hao ambao wamekataa kula chakula huenda wakafa na kusababisha fujo magerezani.
Sheria hiyo mpya imelaaniwa na chama cha madaktari nchini Israeli, ambacho kinaamini kuwa kuwalisha wafungwa chakula kwa nguvu ni mbinu ya mateso na dhulma na ni hatari kimatibabu.
Chama hicho Kimewaomba madkari wa Israeli wasihusike.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment