Pages

Pages

Pages

Saturday 4 July 2015

HII SASA KALI, UKITAKA KUBEBA MIMBA CHINA LAZIMA UOMBE RUHUSA!

Mwakamke mja mzito China
Kampuni moja ya Uchina inapanga kutoa masharti ambapo wafanyikazi wake watatakiwa kupata ruhusa kabla ya kuanza familia.
Sheria hizo zimechapishwa na kuzua malalamiko mengi katika mitandao.
Sheria kuu inaelezea kwamba wanawake wote walio kwenye ndoa lazima wawe wamehudumu kwa mwaka mmoja kwenye kampuni hiyo kabla ya kutuma kibali cha kukubaliwa kushika mimba.
null
Anayekiuka masharti mapya na kushika mimba anatozwa faini, aidha hapati madakara
Yeyote atakayeshika mimba kinyume cha sheria hiyo atatozwa faini na kunyimwa madaraka yoyote, hata kama amefuzu.
Shirika la utangazaji nchini China limekosoa vikali kampuni hiyo iliyoko mkoa wa Henan na kusema haina ubinadamu kwa wafanyikazi wake.
Muingilio wa masuala binafsi China ni jambo rasmi, hasa sheria ya mtoto mmoja iliyowekwa na serikali miaka ya sabini. Hii iliwalazimisha wazazi kupata mtoto mmoja pakee.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment