Pages

Pages

Pages

Wednesday 1 July 2015

BENDERA AIPONGEZA TFF

Joel Bendera

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dokta Joel Bendera ameipongeza TFF kwa kuandaa mashindano ya ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 13 (U-13),  na maandalizi ya timu hiyo kwa ajili ya kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika za vijana chini ya miaka 17 zitakazofanyika mwaka 2019 nchini Tanzania.

Bendera amesema hiyo ndiyo njia sahihi ya kuelekea kwenye mafanikio pia amepongeza juhudi za Chama cha Soka mkoa wa Manyara na TFF kwa kuandaa kozi za makocha na waamuzi, akisema huo ndiyo uwekezaji mkubwa katika maendeleo ya soka mkoani Manyara.

Aidha aliwaasa makocha kutumia mbinu za kisasa za ufundishaji soka walizozipata kwenda kuendeleza vipaji vya wachezaji watakaowafundisha.

Pia Bendera amewahakikishia wakazi wa Manyara atahakikisha wanaandaa vipaji vitakvyowawezesha kuwa na timu bora itakayowakilisha mkoa wa Manyara.


ACCREDITATION FOR ALL AFRICAN GAMES:
Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) limetangza kufunguliwa kwa maombi ya vitambulilsho kwa wandishi wa habari kwenye fainali za michezo ya Afrika zitakazofanyika mwezi Septemba mwaka huu nchini Congo- Brazaville.

Waandishi wa habari wanaotajiwa kwenda kufanya kazi kwenye michuano hiyo wanaombwa kufanya maombi ya vitambulisho (Accrediatation) kuanzia Juni 29 mpaka Julai 7 mwaka huu.

Link ya kufanya maombi hayo ni @CAF_Online
Accreditation for African Games Congo 2015 draw




IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

No comments:

Post a Comment